Valentina Tereshkova

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Valentina Tereshkova

Valentina Vladimirovna Tereshkova (Kirusi Валентина Владимировна Терешкова) (* 6 Machi 1937) alikuwa mwanaanga kutoka Umoja wa Kisoveti na mwanamke wa kwanza aliyefika kwenye anga la nje.

Alikuwa mtoto wa mkulima aliyeendelea kusoma uhandisi akafaulu kupita mtihani kwa shule ya wanaanga mwaka 1962.

Tar. 16 Juni 1963 alirushwa kwa chombo cha angani Vostok 6 akazunguka dunia mara 49 akarudi duniani 19 Juni.