Neil Armstrong

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Neil Armstrong (1969)

Neil Armstrong (5 Agosti 193025 Agosti 2012) alikuwa rubani mwanaanga wa Marekani aliyeshuka mwezini mwaka 1969, wa kwanza kabisa kati ya wanadamu wote.

Mwanaanga[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa katika familia ya wakulima kwenye jimbo la Ohio tarehe 5 Agosti 1930.

Baada ya kumaliza shule alijiunga na jeshi ambako alipata mafunzo ya uhandisi na kuwa rubani. Mwaka 1952 alishiriki katika vita vya Korea.

Rubani wa majaribio[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka 1955 aliajiriwa na taasisi kitangulizi ya NASA kama rubani wa majaribio kwa aina mpya za ndege.

Mnamo mwaka 1958 alikuwa mmojawapo katika kundi la marubani waliotayarishwa kupelekwa kwenye anga-nje.

Mwanaanga[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kuundwa kwa NASA aliingia katika kundi la wanaanga. Safari yake ya kwanza ilikuwa 16 Machi 1966 kama mwanaanga kiongozi wa Gemini 8. Kilele cha safari hii ilikuwa kukutana kwa Gemini 8 na satelaiti nyingine na kuunganisha vyombo vyote viwili kwa muda wa masaa kadhaa.

Armstrong akiangalia chombo cha angani mwezini

Safari ya kwenda mwezini[hariri | hariri chanzo]

Baadaye aliteuliwa kuwa makamu wa kikundi cha wanaanga waliokwenda mwezini kwa kutumia chombo kilichoitwa Apollo 11. Ajali ya Apollo 1 iliyosababisha kifo cha mwenzake hapo kabla, ndiyo iliyompelekea kujiunga kwake na kundi la Apollo 11.

Tarehe 20 Julai 1969 Neil Armstrong pamoja na Edwin Aldrin waliukanyaga uso wa mwezi wakiwa wanadamu wa kwanza mwezini. Walitoka katika chombo cha angani na kutembea mwezini kwa mara ya kwanza. Picha hizo zilionyeshwa kote duniani kwa wakati huohuo. Akiwa katika hali hiyo, Armstrong alitamka maneno yafuatayo: "Hii ni hatua ndogo kwa mtu lakini hatua kubwa kwa ubinadamu."

Baada ya kurudi salama, Armstrong aliacha kazi katika NASA na badala yake akawa profesa wa uanaanga kwenye chuo kikuu cha Cincinnati katika mwaka 1971 hadi alipostaafu na kujishugulisha na biashara zake.

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Neil Armstrong kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.