Nenda kwa yaliyomo

Rubani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Marubani wa ndege ya Boeing 777 wakati wa kutua pale Sharm-el-Sheikh, Misri.

Rubani (kutoka Kiarabuː ربان ruban; kwa Kiingerezaː pilot) ni mtu anayeendesha eropleni au chombo kingine cha usafiri hasa chombo cha usafiri kitumiacho njia ya anga.

Neno hili hutumiwa siku hizi kumtaja hasa mwanahewa lakini kwa asili lilimaanisha mtu anayeongoza chombo cha majini.

Kazi hii inahitaji elimu na maarifa maalumu, kwa hiyo kuna sheria na masharti mbalimbali katika nchi zote duniani kwa watu wanaotaka kuingia katika kazi hii.

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rubani kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.