Adhara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Adhara (Epsilon Canis Majoris)
Kundinyota Mbwa Mkubwa (Canis Major)
Mwangaza unaonekana 1.5
Kundi la spektra B2 II
Paralaksi (mas) 7.57 ± 0.57
Umbali (miakanuru) 430
Mwangaza halisi -4.8
Masi M☉ 12.6
Nusukipenyo R☉ 13.9
Mng’aro L☉ 38700
Jotoridi usoni wa nyota (K) 22900
Majina mbadala Adhara, Adharaz, Undara, ε CMa, 21 CMa, ADS 5654, CD −28° 3666, FK5 268, HD 52089, HIP 33579, HR 2618, SAO 172676.


Adhara (Adhara pia ε Epsilon Canis Majoris, kifupi Epsilon CMa, ε CMa) ni nyota angavu ya pili katika kundinyota la Mbwa Mkubwa (Canis Major) na nyota angavu ya 24 kwenye anga ya usiku[1].

Jina

Adhara linalomaanisha “bikira” lilijulikana kwa mabaharia waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. [2]. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wanaosema العذارى al-adhara neno linalomaanisha "bikira" [3]. Kwa matumizi ya kimataifa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia ulikubali jina la kiarabu na kuorodhesha kundinyota hili kwa jina la "Adhara" [4] .

Epsilon Canis Majoris ni jina la Bayer; hapa inaonekana Bayer alifuata mpangilio wa nyota angani na kuiweweka katika nafasi ya tano, maana kwa kawaida Adhara inatajwa kuwa nyota angavu ya pili katika Mbwa Mkubwa.

Tabia

Adhara liko umbali wa miakanuru 470 kutoka Jua letu lilipo na ni mfumo wa nyotamaradufu. Kundiyota kuu ni Adhara A lililo na mwangaza unaoonekana wa 1.5 na mwangaza halisi ni -4.8. Spektra yake ni ya aina ya B2. Kundinyota la pili B lina mwangaza unaonekana wa 7.5.

Miaka milioni 4.5 – 5 iliyopita Adhara lilikuwa nyota angavu kabisa kwenye anga ya Dunia. Wakati ule umbali wake kutoka kundinyota hilo lilipo hadi kwenye Jua ulikuwa miakanuru 34 pekee na mwangaza wake ulioonekana kuwa -3.99.[5]

Kutokana na jotoridi kubwa kwenye uso wake, sehemu kubwa ya mng’aro wake unatoka kwenye spektra ya urujuanimno (ultraviolet radiation) na Adhara ni chanzo kikubwa cha mnururisho huu angani[6].

Tanbihi

 1. Canis Major - Adhara – ε Canis Majoris tovuti ya constellation guide
 2. ling. Knappert 1993
 3. Kiasili al-adhara ilimaanisha nyota nne za ε, δ, η na ο – Allen (1899), uk. 130
 4. Naming Stars, tovuti ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia (Ukia), iliangaliwa Novemba 2017
 5. Tomkin, Jocelyn (April 1998)
 6. Wilkinson, E.; Green, J. C.; McLean, R.; Welsh, B. (1996)

Viungo vya Nje


Marejeo

 • Allen, Richard Hinckley: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 59 (online kwenye archive.org)
 • Knappert, Jan: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331
 • Lane, Edward William : An Arabic - English Lexicon by in eight parts – 1872 (Perseus Collection Arabic Materials Digitized Text Version v1.1 of reprint Beirut – Lebanon 1968) online hapa
 • Tomkin, Jocelyn (April 1998). "Once and Future Celestial Kings" (PDF). Sky and Telescope. 95 (4): 59–63.
 • Wilkinson, E.; Green, J. C.; McLean, R.; Welsh, B. (1996). "Extreme Ultraviolet Spectrum of ɛ Canis Majoris Between 600-920 Å". Bull. Am. Astron. Soc. 28 (2): 915 online hapa