Mng'aro wa Jua

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka L☉)
Jump to navigation Jump to search
Kiwango cha nishati kinachofika kwenye sehemu fulani kutoka chanzo S kinategemea umbali wake na chanzo.

Mng'aro wa Jua (ing. luminosity of the Sun) ni jumla ya mng'aro au mnururisho wa sumakuumeme unaotoka kwenye Jua na kuelekea nje yake katika anga-nje kwa pande zote. Hii ni pamoja na wimbiredio, mikrowevu, mawimbi ya joto, eksirei, na nuru inayoonekana kwetu.

Mng'aro huu huwa na kiwango cha nishati cha Joule 1367 kinachofika kwa kila mita ya mraba katika umbali wa kizio astronomia moja (= kilomita milioni 150, sawa na umbali wa Dunia kutoka Jua).

Hali halisi kiwango cha nishati kutoka Jua kinachofika kwenye uso wa ardhi kinaweza kuwa chini yake; maana uso wa Dunia haukai wima kwa Jua bali unanama kwa pembe fulani inayobadilika katika mwendo wa mwaka; mabadiliko ya pembe ya mng'aro wa Jua ni sababu ya kuwa na majira ya joto na baridi duniani.

Mng'aro wa Jua kama kipimo cha astronomia[hariri | hariri chanzo]

Kiasi cha nishati ya Jua inayofika kwa umbali wa kizio astronomia moja, yaani takriban kwa umbali wa Dunia kutoka Jua kinatumiwa kama kipimo cha ulinganishi wa nyota.

Hapo mnururisho wote wa nyota unaopimwa unalinganishwa na mng'aro wa Jua. Alama yake ni .