Mwangaza halisi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Mwangaza halisi (kwa Kiingereza absolute magnitude) ni kipimo cha ukali wa nuru ya nyota au magimba mengine ya anga jinsi ilivyo kwa umbali sanifu wa miaka ya nuru 32.6 au parsek 10.

Mwangaza halisi ni tofauti na mwangaza unaoonekana jinsi tunavyoona nyota kutoka Dunia. Maana mwangaza tunaoona unategemea na ukubwa wa nyota, umbali wake na mambo mengine. Nyota ndogo na hafifu iliyo karibu nasi katika anga la nje itaonekana angavu kushinda nyota kubwa iliyo mbali. Hii ni sawa na kuangalia taa iliyo karibu au mbali.

Kipimo hiki kinawaruhusu wanaastronomia kulinganisha uangavu wa magimba kwa kutumia umbali sanifu.

Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwangaza halisi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.