Nenda kwa yaliyomo

Vega

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Vega (Alpha Lyrae)
Nyota Vega katika Shaliaki (Lyra)
Kundinyota Kinubi (Lyra)
Mwangaza unaonekana +0.026
Kundi la spektra A0 Va
Paralaksi (mas) 130.23 ± 0.36
Umbali (miakanuru) 25
Mwangaza halisi +0.582
Masi M☉ 2.13
Nusukipenyo R☉ 2.3
Mng’aro L☉ 40.12
Jotoridi usoni wa nyota (K) 9600
Muda wa mzunguko masaa 12.5
Majina mbadala Wega, Lucida Lyrae, Alpha Lyrae, α Lyrae, 3 Lyr, BD+38°3238, GCTP 4293.00, HD 172167, GJ 721, HIP 91262, HR 7001, LTT 15486, SAO 67174


Vega au α Alfa Lyrae ni nyota angavu zaidi katika kundinyota la Shaliaki (kwa Kiingereza Lyra) na kati ya nyota angavu sana kwenye anga ya usiku.

Jina linatokana na Kiarabu النسر الواقع al-nasr al-waqi, hasa kutoka sehemu ya pili واقع ambamo herufi ya ق q ilichukuliwa kama "g" na hivyo kuleta "Vega" kwa tahajia ya Kilatini. Hili ni jina lililokubaliwa na Umoja wa Kimataifa wa Astronomia[1].

Vega ni nyota ya safu kuu inayoyeyunganisha hidrojeni kuwa heliamu ndani ya kiini chake. Masi yake ni zaidi ya mara mbili ya masi ya Jua. Ilhali nyota kubwa huchoma fueli yake ya myeyungano haraka kuliko nyota ndogo zaidi Vega itakuwa na maisha mafupi kuliko Jua. Kwa sasa mwangaza halisi ni mara kumi ya Jua. Inazunguka haraka kwenye mhimili wake.

Hadi sasa sayari zinazozunguka Vega hazikuthibitishwa. Lakini kuna dalili ya kwamba kuna mata inayozunguka nyota iliyo katika mchakato ya kujikaza kuwa sayari [2]

  1. Naming Stars, tovuti ya Ukia, iliangaliwa Oktoba 2017
  2. Astronomers discover possible new Solar Systems in formation around the nearby stars Vega and Fomalhaut, tovuti ya outreach.jach.hawaii.edu, iliyohifadhiwa kwa archive.org, iliangaliwa Oktoba 2017

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
  • Vega, tovuti ya prof Jim Kaler, university of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vega kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.