Zodiaki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Ukanda wa Zodiaki angani, picha iliyochorwa katika kuba ya kanisa la Italia, ikionyesha mstari wa njia ya Jua kati ya kundinyota za ekliptiki

Zodiaki ni kanda kwenye anga lenye upana wa takriban nyuzi 20 linalofuata mstari wa ekliptiki yaani mstari wa njia dhahiri ya Jua angani katika mwendo wa mwaka mmoja. Mstari huu unapatikana kwa kutazama Jua wakati wa mapambazuko ambako linaonekana katika mazingira ya kundinyota tofauti. Kila mwaka Jua linapambazuka katika eneo la kundinyota zilezile.

Njia dhahiri za Mwezi na sayari zinaonekana pia katika kanda hili la zodiaki.

Hadi leo unajimu unatumia kundinyota hizi 12 kama buruji za falaki kwa imani ya kwamba nyota hizi zina athira kwa kipindi fulani cha mwaka kinachoitwa kufuatana na kundinyoti au buruji ya falaki yake. Lakini hali halisi Jua linapita katika maeneo ya kundinyota 13, si 12.

Miaka 3000 iliyopita ambako mfumo wa Zodiaki ulibuniwa, wataalamu wa Babeli waliondoa kundinyota ya Hawaa (Ophiuchus) katika mfumo kwa shabaha ya kupata mgawanyo wa anga unaolingana na miezi 12 ya kalenda.

Kumetokea pia badiliko ya kwamba kundinyota za Zodiaki hazilingani tena na vipindi vya mwaka ambako zinatangazwa na wanajimu wa leo. Sababu yake ni kusogea kwa mhimili wa Dunia na hii inasababisha ya kwamba sisi tunatazama anga kwa pembe tofauti kuliko wazee miaka 2000 iliyopita. Ila tu wanajimu wanaendelea kutumia vipindi vilivyopimwa zamani ile.


Kundinyota za ekliptiki[hariri | hariri chanzo]

Jedwali ifuatayo inaonyesha hali halisi ya kundinyota 13 zinazopitiwa na Jua katika mwendo wa mwaka mmoja. Kwa sasa nukta ya machipuo iko ndani ya Hutu (Pisces) hivyo hapa iko nafasi ya 0°


Kundinyota Ishara Nafasi kwenye
ekliptiki
Kipindi cha kupita
kwa Jua (mwaka 2010)
Kipindi cha Buruji ya Falaki
inayolingana katika unajimu
Kiswahili Kilatini
Hamali (Kondoo) Aries Hamali 28,8°–53,5° 19. Apr – 14. Mei 21 Machi- 19 Mei
Thauri (Ng’ombe) Taurus Thauri 53,5°–90,2° 14 Mei – 21 Juni 20 Aprili – 21 Mei
Jauza (Mapacha) Gemini Jauza 90,2°–118,1° 21 Juni– 20. Julai 22 Mei – 20 Juni
Saratani (Kaa) Cancer Saratani 118,1°–138,2° 20 Julai – 11. Agosti 21 Juni – 22 Julai
Asadi (Simba) Leo Löwe 138,2°–173,9° 11 Agosti – 17. Sept 23 Julai – 22 Agosti
Nadhifa (Mashuke) Virgo Nadhifa 173,9°–218,0° 17 Sept – 31 Okt 23 Agosti – 22 Sept
Mizani Libra Mizani 218,0°–241,0° 31 Okt – 23 Nov 23 Sept – 23 Okt
Akarabu (Nge) Scorpius Akarabu 241,0°–247,7° 23 Nov – 30 Nov 24 Okt – 21 Nov
Hawaa Ophiuchus Hawaa 247,7°–266,3° 30 Nov – 18 Des (ilifutwa katika unajimu)
Kausi au Mshale Sagittarius Kausi 266,3°–299,7° 18 Des – 20 Jan 22 Nov – 21 Des
Jadi au Mbuzi Capricornus Jadi (Capricornus) 299,7°–327,6° 20 Jan – 16 Feb 22 Des – 19 Jan
Dalu au Ndoo Aquarius Dalu (Aquarius) 327,6°–351,6° 16 Feb – 12 Machi 20 Jan – 18 Feb
Hutu au Samaki Pisces Hutu (Pisces) 351,6°–28,8° 12 Machi – 19 Apr 19 Feb – 20 Machi

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Sciences de la terre.svg Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Zodiaki kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.