Buruji za falaki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Buruji za falaki katika muswada ya Kiosmani, karne ya 16
Uchoraji wa Kausi (hapa kwa jina mbadala "al-Rami") katika muswada ya Al-Sufi "Kitāb Ṣuwar al-kawākib (al-thābitah)" , mnamo mwaka 1006

Buruji za falaki (ing. zodiac constellations) ni jina kwa kundinyota zinazoonekana kwenye mstari wa njia ya jua angani (ing. ecliptic).

Katika elimu ya unajimu (au: falaki, tofauti na astronomia) Waswahili wa kale, pamoja na tamaduni nyingi za zamani, waliamini ya kwamba nyota hizi zina tabia fulani na kuna athira juu ya maisha ya binadamu wanaozaliwa chini ya nyota.

Jina[hariri | hariri chanzo]

Kwa jumla majina mengi ya nyota yametokana na urithi wa falaki ya Waarabu. Hao wenyewe walirithi habari hizi pamoja na mpangilio wa nyota kwenye mzingo wa njia ya jua angani kutoka Ugiriki ya Kale. Asili yake iko katika falaki ya Babeli. "Buruji" yatokana na Kiarabu "برج" (burj, tafsiri ya gir. πυργοι pirgoi) yaani mnara au boma[1].

Buruji za falaki kwenye njia ya jua angani[hariri | hariri chanzo]

Buruji za falaki katika utamaduni wa Waswahili ni kama zifuatazo:[2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Hakuna uhakika juu ya maana ya kiasili ya jina hili; Hartner-Kunitsch katika makala MINTAKAT AL-BURUDJ wanarejelea elezo kuwa asili iko katika mitolojia ya Babeli kwa maana "makazi ya miungu"; tazama kamusi elezo ya Uislamu "The Encyclopaedia Of Islam, New Edition", Volume VII Mif — Naz
  2. J Knappert, fungu "In East Africa", makala AL-NUDJUM katika THE ENCYCLOPAEDIA OF ISLAM, LEIDEN BRILL 1997, VOLUME VIII NED — SAM, uk 105