Astronomia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Falaki)
Rukia: urambazaji, tafuta
Aina mbalimbali za darubini ni vyombo muhimu ya astronomia

Astronomia (kutoka Kigir. ἄστρον astron "nyota" na νόμος nomos "sheria")[1] ni elimu juu ya magimba kwenye ulimwengu kama vile nyota, sayari, miezi, vimondo, nyotamkia, galaksi kuhusu nyendo zao, nafasi, umbali, ukubwa na sheria zinazotawala tabia zao.

Astronomia ni tofauti na unajimu ambayo si sayansi bali jaribio la kuona uhusiano kati ya nyota na tabia za wanadamu pia kutabiri mambo yajayo.

Chanzo na historia ya astronomia[hariri | hariri chanzo]

Tangu zamani watu walitazama mabadiliko kati ya nyota zinazoonekana angani wakati wa usiku. Walitazama pia ya kwamba mabadiliko mengi yanarudia kila mwaka na yana uhusiano na nyakati za mvua, baridi na joto, mavuno na ustawi wa mimea katika mwendo wa mwaka. Kutazama nyota vile kulikuwa msaada wa kupanga vipindi vya mwaka na kuunda kalenda. Watazamaji wa nyota walianza kutambua pia tofauti kati ya nyota mbalimbali kwa mfano nyota zenye mahali palepale kila wakati na nyota chache za pekee zilizobadilisha mahali angani kwa utaratibu wa kurudia na hizi ziliitwa sayari, tena nyota nyingine zilizoonekana kwa muda tu zikibadilisha mahali pao angani zikaitwa vimondo.

Kwa karne nyingi wataalamu katika sehemu mbalimbali za dunia walihisi ya kwamba nyota hizi zilikuwa miungu zilioonekana kwa mbali sana. Katika vitabu vya kidini vya kale kuna majadiliano juu ya tabia zao; wakati mitholojia ya mataifa mengi iliona nyota kuwa miungu Biblia ilifundisha ni taa zilizowekwa na Mungu wa pekee mwumbaji wa ulimwengu.

Wataalamu wa kale katika nchi kama Uhindi au Ugiriki ya Kale walianza kutambua mwendo wa sayari na kuunda nadharia yuu ya uhusiano wa dunia, jua na sayari nyingine.

Tangu kupatikana kwa vyombo vya utazamaji nyota vilivyoboreshwa kama darubini elimu halisi juu ya nyota na sayari ilisogea mbele.

Siku hizi wataalamu wameelewa tabia za nyota nyingi kuwa magimba kama jua letu wakati sayari kuwa magimba kama dunia yetu yanayozunguka jua letu katika mfumo wa jua. Wameelewa pia ya kwamba kuna mabilioni ya nyota zinazojumika pamoja katika makundi makubwa yanayoitwa galaksi.

Vyombo vya utazamaji vilivyopatikana katika karne ya 20 vilionyesha magimba yasiyoonekana kwa macho kwa sababu hayana nuru ya kawaida bali yanafikisha kwetu mnururisho ya mawimbi ya redio tu.

(itaendelea)

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Awali makala iliitwa "Falaki"(kutoka Kar. علم الفلك 'ilm al-falak "elimu ya mizingo ya magimba ya angani") lakini kwa kufuata ushauri wa Dr Noorali T Jiwaji, Open University of Tanzania ilionekana ya kwamba wataalamu wa fani hii katika Tanzania walipatana kutumia neno "Astronomia".

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Astronomia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.