Galaksi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Galaksi ya Andromeda yenye na. M 31 na galaksi mbili ndogo za kando M 32 na M 110

Galaksi ni kundi la nyota nyingi zinazoshikamana pamoja katika anga la ulimwengu kutokana na graviti yao. Nyota hupatikana angani katika makundi kama mawingu makubwa sana.

Kuna galaksi nyingi sana ulimwenguni. Kwa wastani kila galaksi imekadiriwa kuwa na nyota kama bilioni 100 lakini kuna galaksi kubwa na ndogo.

Galaksi yetu, ikiwemo mfumo wa jua letu, imekadiriwa kuwa na nyota zaidi ya 300,000,000,000. Sehemu ya nyota hizi zinaonekana kama kanda la kung'aa kwenye anga la usiku linalojulikana kwa rangi yake kama njia nyeupe au njia ya maziwa (kiowevu hicho kwa Kigiriki kinaitwa "galax"). Umbo lake unafanana na kisahani kikiwa na kipenyo cha miaka ya nuru 100,000 na kikiwa na unene wa miaka ya nuru 3,000.

Galaksi iliyo karibu angani inaitwa Andromeda na ina umbali wa miaka ya nuru milioni 2.5.

Idadi kamili ya galaksi zote angani haijulikani. Kuna makadirio ya kwamba idadi ya galaksi bilioni inaweza kuangaliwa kwa vyombo vinavyopatikana. Hadi sasa sehemu ndogo tu imehesabiwa lakini mara kwa mara galaksi mpya zinatambuliwa kwa njia ya darubini au vyombo vya angani.

Galaksi zinazojulikana zimepewa namba katika orodha ya kimataifa ya wanasayansi wa astronomia.

Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Galaksi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.