Mawingu ya Magellan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mawingu ya Magellan

Mawingu ya Magellan (ing. Magellanic Clouds) ni galaksi mbili ndogo zinazoonekana kwa macho matupu kama doa angavu angani kwa watazamaji kwenye nusutufe ya kusini ya Dunia. Hazionekani kwenye nusutufe ya kaskazini.

Mawingu ya Magellan ni sehemu ya kundi janibu la galaksi yakizunguka Njia Nyeupe. Hayana umbo maalum. Yanaitwa

  • Wingu Kubwa la Magellan (Large Magellanic Cloud - LMC) lina umbali wa miaka ya nuru 170,000 kutoka kwetu na idadi ya nyota ni takriban bilioni 15
  • Wingu Dogo la Magellan (Small Magellanic Cloud - SMC) lina umbali wa miaka ya nuru 200,000 kutoka kwetu na idadi ya nyota ni takriban bilioni 5

Mawingu haya yalijulikana tangu kale kati ya mataifa ya nusutufe ya kusini na kupokea majina. Ushuhuda wa kwanza wa kimaandishi upo katika kitabu cha mwanaastronomia Al Sufi katika kitabu chake juu ya nyota mnamo mwaka 964 BK. Mzungu wa kwanza aliyeyaeleza alikuwa Ferdinand Magellan alipozunguka Dunia kwenye mwaka 1519.

Katika darubini, mawingu yanaonekana kama galaksi yenye nyota, nebula na fungunyota ndani yake.

Astrowiki.PNG
Mradi wa Astronomia

Makala hii imewahi kukaguliwa na kuboreshwa kwenye warsha ya pamoja ya Jenga Wikipedia ya Kiswahili, Wikimedia Community User Group Tanzania na ASSAT. Imepewa hali ya ulinzi. Tunaomba mapendekezo yote ya usahihisho na nyongeza zipelekwe kwanza kwenye ukurasa wa majadiliano