Njia nyeupe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Njia nyeupe jinsi inavyoonekana usiku (Mistari mekundu inaonyesha mipaka yake; sehemu ya chini imefichwa na mti)
Galaksi yetu jinsi inaaminiwa kuonekana vile kama tunaiangalia kutoka juu; picha ya galaksi ya mbali yenye mikono miwili ya parafujo

Njia Nyeupe (ing. Milky Way), pia majarra au "mkokoto wa kondoo za Sumaili" [1] ni jina la kanda ya nyota nyingi inayoonekana wakati wa usiku angani kama wingu nyeupe inayong`aa.

Hali halisi hii ni jinsi tunavyoona galaksi yetu ambamo jua letu na mfumo wake ni sehemu yake.

Galaksi yetu imekadiriwa kuwa na nyota zaidi ya 300,000,000,000. Umbo lake unafanana na kisahani chenye umbo la parafujo. Kipenyo cha kisahani hiki ni miaka ya nuru 100,000 ikiwa na unene wa miaka ya nuru 3,000. Galaksi ya jirani iliyo karibu angani inaitwa Andromeda na ina umbali wa miaka ya nuru milioni 2.5 .

Kuonekana kwa Njia Nyeupe kutoka duniani[hariri | hariri chanzo]

Nyota karibu zote tunazoona kwa macho yetu wakati wa usiku ni sehemu za Njia Nyeupe. Wakati wa giza tunaweza kuona kati ya nyota 3,000 hadi 5,000 kwa macho yetu bila msaada wa darubini. Isipokuwa sayari za jua letu na kometi (zinazoonekana mara chache tu) na galaksi ya Andromeda (inayoonekana kama nyota 1) nyota zote ni majua kama jua letu. Si rahisi kuona nyota nyingi tukiwa mjini penye nuru nyingi wakati wa usiku kwa sababu mwanga wa taa za mjini unaakisiwa katika angahewa na kuleta matata ya kuona mwanga kutoka nje ya angahewa.

Nyota zilizo nyingi za Njia Nyeupe hatuwezi kuziona wala kubainisha kwa hiyo zinatokea machoni kama ukungu mweupe tu.

Uwezo wetu kuona nyota nyingi umepungukiwa na kuwepo kwa mavumbi ya kinyota kati ya mahali petu na kitovu cha galaksi.

Muundo[hariri | hariri chanzo]

Galaksi yetu ina umbo la parafujo (spirali) ya kisahani. Mahali petu pamoja na jua pako kando kiasi ndani ya uwiano wa kisahani hiki. Tuko takriban 2/3 ya umbali wa kipenyo kutoka kitovu cha kisahani.

Ikitazamiwa kutoka juu galaksi yetu ina umbo la parafujo lenye mikono mbalimbali. Picha hii tumepata kutokana na kuangalia galaksi za mbali angani zinazoonekana kutoka juu na parafujo inaonekana.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. yaani njia ya kondoo wa Ismaili; kuhusu majina ya nyota na sayari zilizojulikana kwa Waswahili na hivyo kuwa na majina asilia linganisha Jan Knappert, Swahili Islamic poetry, Brill 1971, Vol 1 uk 96-97 - taz google booksearch [1]

Soma pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: