Shimo jeusi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Uchoraji wa shimo nyeusi jinsi wataalamu wanaiwaza. Hadi leo hakuna picha halisi ya shimo nyeusi.

Shimo jeusi (Kiingereza: black hole) ni jina kwa eneo kwenye anga ya ulimwengu lenye graviti kubwa kiasi kwamba hata nuru haiwezi kutoka nje yake. Nadharia ya uhusianifu inatabiri ya kwamba gimba lenye masi kubwa iliyokandamizwa katika eneo dogo litasababisha "shimo jeusi". Eneo hili lazungukwa na upeo usioonekana lakini mipaka ya upeo huu ni kama mstari ambao kila kitu kinachoupita hakiwezi kurudi tena kwa sababu kinavutwa mno na graviti ya shimo jeusi. Eneo hili laitwa "jeusi" kwa sababu nuru yote inayofika upeo huu inamezwa kabisa hakuna inayorudishwa tena.

Kwa hiyo hadi sasa haikuwezekana kutazama shimo jeusi moja kwa moja. Lakini wataalamu wa fizikia waliwahi kuyatabiri mashimo haya.

Katika miaka ya nyuma astronomia imeangalia mahali pengi ambako mwendo wa nyota za eneo fulani si kawaida unaelezwa kwa kuwepo kwa shimo jeusi katika sehemu hizi maana yake graviti yake inaathiri mwendo wa nyota au mawingu ya gesi ya angani na kuzivutia kwake. Mwendo huu wa magimba katika mazingira ya mashimo meusi unaonekana kwa wanaastronomia.

Inaaminiwa ya kwamba shimo jeusi linatokea wakati wa kufa kwa nyota kubwa lenye masi inayozidi masi ya jua letu mara tatu au zaidi.

Astrowiki.PNG
Mradi wa Astronomia

Makala hii imewahi kukaguliwa na kuboreshwa kwenye warsha ya pamoja ya Jenga Wikipedia ya Kiswahili, Wikimedia Community User Group Tanzania na ASSAT. Imepewa hali ya ulinzi. Tunaomba mapendekezo yote ya usahihisho na nyongeza zipelekwe kwanza kwenye ukurasa wa majadiliano