Saratani (kundinyota)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Kwa ugonjwa yenye jina hili angalia hapa Saratani

Nyota za kundinyota Saratani (Cancer) katika sehemu yao ya angani
Ramani ya Saratani - Cancer jinsi inavyoonekana kwa mtazamaji kwenye nusutufe ya kaskazini

Saratani (pia: Kaa au Cancer[1] kwa Kilatini/Kiingereza) ni kundinyota ya zodiaki. Ni moja ya kundinyota zinazotambuliwa na Umoja wa Kimataifa wa Astronomia [2]

Nyota za Saratani huwa haziko pamoja kihalisi lakini zinaonekana tu vile kutoka duniani. Kwa uhalisi kuna umbali mkubwa kati yao, kama ziko mbali au jirani nasi. Kwa hiyo kundinyota "Saratani" inaonyesha eneo la angani jinsi tunavyoiona kutoka Duniani.

Jina[hariri | hariri chanzo]

Saratani ilijulikana kwa jina hili kwa miaka mingi kati ya mabaharia Waswahili waliotumia nyota kutafuta njia baharini wakati wa usiku.[3]

Jina la Saratani linatokana na Kiarabu سرطان sartan linalomaanisha kaa[4]. Jina hili lilipokelewa na Waarabu kutoka kwa Wagiriki wa Kale waliosema Καρκίνος karnikos kwa maana hiyohiyo na hao walipokea kundinyota hii tayari kutoka Babeli lakini Wababeli waliiona kama alama ya kobe maji.

Katika unajimu wa kisasa katika Afrika ya Mashariki jina "Saratani" limesahauliwa ikiwa kundinyota inaitwa kwa tafsiri tu "Kaa".

Katika vitabu kadhaa vya shule jina la Saratani limetumiwa kutaja sayari ya Zohali kwa kulichanganya na matamshi ya jina la Kiingereza "Saturn".

Jina la kundinyota hili ni sawa na ugonjwa wa saratani unaoitwa pia "kansa". Sababu yake ni ya kwamba matibabu wa kale walifananisha uvimbe wa ugonjwa na mnyama kaa na hili ni pia maana ya neno saratani.

Mahali pake[hariri | hariri chanzo]

Saratani iko angani kwenye mstari wa Zodiaki kati ya Jauza (Gemini) upande wa magharibi na Asadi (Leo) upande wa mashariki.

Magimba ya angani[hariri | hariri chanzo]

Saratani haina nyota angavu sana si rahisi kuiona. Nyota angavu zaidi ni Beta Cancri yenye mwangaza unaoonekana wa 3.8 mag. Umbali wake na dunia ni miaka ya nuru 230. Kuna fungunyota moja inayoonekana kwa macho matupu hii ni M 44 inayoitwa pia Praesepe yenye mwangaza unaoonekana wa 3.7 ikionekana kama doa dogo angavu.

Jina la
(Bayer)
Namba ya
Flamsteed
Jina
(Ukia)
Mwangaza
unaoonekana
Umbali
(miaka ya nuru)
Aina ya spektra
β 17 Acubens 3,53m 230 K4 III
δ 47 Asellus Australis 3,94m 150 K0 III
ι 48 3,9 m 300 G6 + A3
α 65 Acubens 4,26m 180 A3
γ 43 Asellus Borealis 4,66m 160 A1 V
ζ 16 Tegmine 4,7 ca. 82 F7 V + F9 V + G0 V + M

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Cancer" katika lugha ya Kilatini ni "Cancris" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Cancris, nk.
  2. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017
  3. ling. Knappert 1993
  4. Ugonjwa wa saratani au kansa ulipokea jina lake kwa sababu matibabu wa Ugiriki ya Kale waliona uvimbe wake unafanana na miguu ya mnyama kaa.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Ian Ridpath and Wil Tirion (2007). Stars and Planets Guide, Collins, London. ISBN 978-0007251209. Princeton University Press, Princeton. ISBN 978-0-691-13556-4.
  • Dictionary of Symbols, by Carl G. Liungman, W. W. Norton & Company. ISBN 978-0-393-31236-2
  • Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 107 ff (online kwenye archive.org)
  • Jan Knappert, 1993: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331Lübeck 2012 (96).jpg Kundinyota za Zodiaki Cal zod.jpg

Akarabu (Nge) - Scorpius * Asadi (Simba) - Leo * Dalu (Ndoo) - Aquarius * Hamali (Kondoo) - Aries * Hutu (Samaki) - Piscis * Jadi (Mbuzi) - Capricornus * Jauza (Mapacha) - Gemini * Kausi (Mbuzi) - Capricornus * Mizani - Libra * Nadhifa (Mashuke) - Virgo * Saratani (Kaa) - Cancer * Tauri (Ng'ombe) - Taurus *