Nenda kwa yaliyomo

Sumbula

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sumbula (Spica) katika kundinyota la Nadhifa (Virgo)

Sumbula (kwa Kiingereza na Kilatini Spica spi-ka, pia α Alpha Virginia, kifupi Alpha Vir, α Vir) ni jina la nyota angavu zaidi katika kundinyota la Nadhifa (en:Virgo) ikiwa pia nyota angavu ya 15 kwenye anga la usiku.

Jina

Jina la kimataifa ni en:Spica, pamoja na Alpha Virginis[1]. Jina la Kiswahili linatokana na Kiarabu السنبلة al-sunbula[2]. Maneno yote humaanisha "shuke" (mbegu za nafaka) na asili ni unajimu wa Babeli ambako watu waliabudu mungu wa kike wa kilimo waliyemwita shala shubultu yaani Mungu wa Shuke na kumtabua katika nyota akishika shuke mkononi. Kundinyota hili lilipokewa na Wagiriki wa Kale na kutoka huko na Waarabu.

Tabia

Sumbula iko kwa umbali wa miakanuru 250 ± 10 kutoka jua letu. Katika darubini inaonekana si nyota 1 bali nyota mbili zilizo karibu sana na kuzungukana. Kwa sababu hiyo uangavu wa Sumbula unachezacheza kiasi, maana mara tunaona sehemu ya kiangavu zaidi mbele, mara sehemu ya kiangavu kidogo.

Marejeo

  1. Naming Stars, tovuti ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia (Ukia), iliangaliwa Novemba 2017
  2. Ling makala "Mintakat al-burudj" katika Encyclopaedia of Islam , Volume 6, uk 87, New Edition ed. Clifford Edmund Bosworth, Brill Archive, 1986 ISBN 9004078193, 9789004078192
    Kamusi za KKS na Kamusi Kuu pamoja na vitabu kadhaa za shule zinaorodhesha "Sumbula" kama kisawe cha Mshtarii (sayari), ambayo inaonekana kama mchanganyo; chanzo cha mapema zaidi kwa kosa kinapatikana kwenye kamusi ya KAST (1995)
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sumbula kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.