Shuke

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kwa matumizi ya neno hili kutaja kundinyota angalia Mashuke (kundinyota)

Mashuke yasiyoiva bado ya shayiri, ngano na ngano nyekundu

Shuke (pia: suke, ing. ear) ni sehemu ya shina ya mmea wa nafaka penye mbegu, kama vile mtama, mpunga au ngano penye mbegu. Kwahiyo ni sehemu yenye zao la nafaka.

Shuke inaanza kama fungu la maua yanayokaa pamoja kwenye sehemu ya shina ya nyasi. Maua haya yanaendelea kuwa matunda yenye mbegu. Mbegu kwa kawaida ni kusudi la kulima mmea na hivyo mashuke ni sehemu za thamani zaidi ya mimea wakati inapovunwa.

Njia ya kuvuna ni mara nyingi kukata mashina ya nafaka na kutikisisha au kupiga mashuke hadi mbegu zinaachana na shina na kuzikusanya pekee.

Mashuke hutokea pia kwa manyasi mengine yasiyotumiwa kama nafaka.