Nenda kwa yaliyomo

Ngano nyekundu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ngano nyekundu
(Secale cereale)
Ngano nyekundu
Ngano nyekundu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Planta (mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Monocots (Mimea ambayo mche wao una jani moja tu)
(bila tabaka): Commelinids (Mimea kama kongwe)
Oda: Poales (Mimea kama manyasi)
Familia: Poaceae (Mimea iliyo na mnasaba na nyasi)
Jenasi: Secale
Spishi: S. cereale
L.
Secale cereale

Ngano nyekundu (lat. Secale cereale; ing. rye) ni mmea wa familia ya manyasi katika ngeli ya monokotiledoni. Mbegu au punje za ngano nyekundu ni nafaka ambayo ni chakula muhimu katika sehemu za dunia hasa kwenye kanda zisizo na joto au baridi kali. Ni mmea ulio karibu na ngano.

Matumizi yake ni kwa ajili ya unga, mkate, bia, aina za wiski na pombe mbalimbali halafu lishe ya wanyama.

Ngano nyekundu hustawi kwenye ardhi ya mchanga ambako ngano haiendelei vizuri inavumilia pia tofauti kubwa zaidi za mvua na ukame kuliko ngano.

Kilimo chake na matumizi[hariri | hariri chanzo]

Nchi walima wakuu wa ngano nyekundu — 2005
(millioni t³)
Urusi 3.6
Poland 3.4
Ujerumani 2.8
Belarusi 1.2
Ukraine 1.1
China 0.6
Kanada 0.4
Uturuki 0.3
Marekani 0.2
Austria 0.2
Dunia 13.3
Habari za FAO[1]


Ngano nyekundu hulimwa hasa katika nchi za Ulaya ya Mashariki, ya kati na kaskazini kama vile Ujerumani, Poland, Ukraine, Belarusi, Lithuania, Latvia hadi Urusi. Hulimwa pia katika Amerika ya Kaskazini (Kanada na Marekani), katika Amerika Kusini (Argentina), Uturuki, Kazakhstan na China ya kaskazini.

Katika Afrika imelimwa kidogo kwenye nyanda za juu za Tanzania pia Kenya.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons