Kombe la Dunia la FIFA 2022

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kombe la Dunia 2022

Kombe la Dunia la FIFA 2022 (kwa Kiarabu :كَأسُ اَلعَالَمِ] 2022, Gulf Arabic: كَاسُ اَلعَالَمِ ٢٠٢٢) ni michuano ya 22 ya Kombe la Dunia la FIFA inayohusisha timu za taifa za wanaume kutoka mataifa mbalimbali katika mchezo wa soka. Michuano hii inashirikisha timu za wanaume kutoka nchi mbalimbali duniani ambazo ni wanachama wa FIFA na hufanyika mara moja kila baada ya miaka minne. Michuano hii imepangwa kufanyika Qatar kuanzia 20 Novemba hadi 18 Desemba 2022[1].

Hili litakuwa Kombe la Dunia la kwanza kufanyika katika nchi za Kiarabu[2] na litakuwa Kombe la Dunia la pili kufanyika katika bara la Asia baada ya mashindano ya 2002 kufanyika nchini Korea Kusini na Japani.[3] Mashindano haya yatakuwa ya mwisho yakihusisha jumla ya timu 32.

Ufikapo mwaka 2026 kutakuwa na ongezeko la jumla ya timu 48. Mabingwa wa Kombe la Dunia mwaka 2018 ilikuwa timu ya taifa ya Ufaransa. [4] Kutokana na majira ya joto nchini Qatar, Kombe hili la Dunia litafanyika kuanzia 20 Novemba hadi 18 Desemba 2022, na kufanya kuwa mashindano ya kwanza kutokufanyika katikati ya mwaka kati ya mwezi Mei, Juni, au Julai.

Timu zilizofuzu

Kufikia tarehe 31 Machi 2022, mataifa 29 yamefuzu kucheza kombe la dunia 2022 ikiwa ni pamoja na mataifa 22 yaliyoshiriki katika mashindano yaliyopita ya mwaka 2018. Qatar ni timu pekee inayocheza mechi yake ya kwanza katika Kombe la Dunia la FIFA, na kuwa wenyeji wa kwanza kucheza mashindano hayo tangu nchini Italia mwaka 1934.[5][6]

Mabingwa mara nne wa Ulaya na washindi wa UEFA Euro 2020, Italia, walishindwa kufuzu kwa mara ya pili mfululizo katika Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika historia yao, walipopoteza nusu fainali za kufuzu dhidi ya Masedonia Kaskazini.[7]

Timu Ya Taifa Kufuzu kama Tarehe ya Kufuzu Idadi ya Miaka Aliyofuzu Kucheza
Kombe La Dunia La Fifa1
Nafasi Aliyofika Katika Mashindano
Ya Kombe la Dunia Yaliyopita
Qatar
Mwenyeji wa mashindano 2 disemba 2010 Mwaka 1 (2022)
Bendera ya Ujerumani Ujerumani Mshindi UEFA kundi J 11 oktoba 2021 miaka 20 (1934, 1938, 1954, 1958, 1962, 1966, 1970, 1974, 1978, 1982, 1986, 1990', 1994, 1998, 2002, 2006, 2010, 2014, 2018, 2022) Mshindi wa kombe la dunia la FIFA mwaka 1954, 1974, 1990, 2014,.
Bendera ya Denmark Denmark Mshindi wa UEFA kundi F 12 oktoba 2021 miaka 6 (1986, 1998, 2002, 2010, 2018,2022) Robo fainali (1998)
Bendera ya Brazil Brazil Mshindi wa kombe la CONMEBOL 11 Novemba 2021 Miaka 22 (1930, 1934, 1938, 1950, 1954, 1958, 1962, 1966, 1970, 1974, 1978, 1982, 1986, 1990, 1994, 1998, 2002, 2006, 2010, 2014, 2018,2022) Mshindi wa kombe la dunia la FIFA mwaka (1958, 1962, 1970, 1994, 2002)
Bendera ya Ufaransa Ufaransa Mshindi wa UEFA kundi D 13 Novemba 2021 Miaka 16 (1930, 1934, 1938, 1954, 1958, 1966, 1978, 1982, 1986, 1998, 2002, 2006, 2010, 2014, 2018,2022) Mshindi wa kombe la dunia la FIFA mwaka (1998, 2018)
Bendera ya Ubelgiji Ubelgiji Mshindi wa UEFA kundi E 13 Novemba 2021 Miaka 14 (1930, 1934, 1938, 1954, 1970, 1982, 1986, 1990, 1994, 1998, 2002, 2014, 2018,2022) Nafasi ya Tatu (2018)
Bendera ya Kroatia Kroatia Mshindi wa UEFA kundi H 14 Novemba 2021 Miaka 6 (1998, 2002, 2006, 2014, 2018, 2022) Runners-up (2018)
Bendera ya Hispania Hispania Mshindi wa UEFA kundi B 14 Novemba 2021 Miaka 16 (1934, 1950, 1962, 1966, 1978, 1982, 1986, 1990, 1994, 1998, 2002, 2006, 2010, 2014, 2018, 2022) Mshindi wa kombe la dunia la FIFA mwaka (2010)
Bendera ya Serbia Serbia Mshindi wa UEFA kundi A 14 Novemba 2021 Miaka 13 (1930, 1950, 1954, 1958, 1962, 1974, 1982, 1990, 1998, 2006, 2010, 2018, 2022) Nafasi ya nne (1930, 1962).
Bendera ya Uingereza Uingereza Mshindi wa UEFA kundi I 15 Novemba 2021 Miaka 16 (1950, 1954, 1958, 1962, 1966, 1970, 1982, 1986, 1990, 1998, 2002, 2006, 2010, 2014, 2018, 2022) Mshindi wa kombe la dunia la FIFA mwaka (1966)
Uswisi
Mshindi wa UEFA kundi C 15 Novemba 2021 Miaka 12 (1934, 1938, 1950, 1954, 1962, 1966, 1994, 2006, 2010, 2014, 2018, 2022) Robo-Fainali (1934, 1938, 1954)
Bendera ya Uholanzi Uholanzi Mshindi wa UEFA kundi G 16 Novemba 2021 Miaka 11 (1934, 1938, 1974, 1978, 1990, 1994, 1998, 2006, 2010, 2014, 2022) Runners-up (1974, 1978, 2010)
Bendera ya Argentina Argentina CONMEBOL runners-up 16 Novemba 2021 Miaka 18 (1930, 1934, 1958, 1962, 1966, 1974, 1978, 1982, 1986, 1990, 1994, 1998, 2002, 2006, 2010, 2014, 2018) Mshindi (1978, 1986)
Bendera ya Uajemi Iran AFC awamu ya tatu, mshindi wa kundi A 27 Januari 2022 Miaka 6 (1978, 1998, 2006, 2014, 2018, 2022) Hatua ya makundi (1978, 1998, 2006, 2014, 2018)
Bendera ya South Korea Korea Kusini AFC awamu ya tatu kundi A - runners-up 1 Februari 2022 Miaka 11 (1954, 1986, 1990, 1994 , 1998, 2002, 2006, 2010, 2014, 2018) Nafasi ya nne (2002)
Bendera ya Japani Japan AFC awamu ya tatu kundi B - runners-up 24 Machi 2022 Miaka 7 (1998, 2002, 2006, 2010, 2014, 2018, 2022) Hatua ya mtoano ya 16 bora (2002, 2010, 2018)
Saudi Arabia
AFC awamu ya tatu, mshindi wa kundi B 24 Machi 2022 Miaka 6 (1994, 1998, 2002, 2006, 2018, 2022) Hatua ya mtoano ya 16 bora (1994)
Bendera ya Jamhuri ya Dominika Jamhuri ya Dominika CONMEBOL - nafasi ya nne 24 Machi 2022 Miaka 4 (2002, 2006, 2014, 2022) Hatua ya mtoano ya 16 bora (2006)
Uruguay
CONMEBOL- nafasi ya tatu 24 Machi 2022 Miaka 14 (1930, 1950, 1954, 1962, 1966, 1970, 1974, 1986, 1990, 2002, 2010, 2014, 2018, 2022) Mshindi wa kombe la dunia la FIFA mwaka (1930, 1950)
Bendera ya Kanada Kanada Mshindi wa CONCACAF awamu ya tatu 27 Machi 2022 Miaka 2 (1986, 2022) Hatua ya makundi (1986)
Bendera ya Ghana Ghana Mshindi wa CAF awamu ya tatu 29 Machi 2022 Miaka 4 (2006, 2010, 2014, 2022) Robo-fainali (2010)
Bendera ya Senegal Senegal Mshindi wa CAF awamu ya tatu 29 Machi 2022 Miaka 3 (2002, 2018, 2022) Robo-fainali (2002)
Ureno
Mshindi wa UEFA awamu ya pili 29 Machi 2022 Miaka 8 (1966, 1986, 2002, 2006, 2010, 2014, 2018, 2022) Nafasi ya tatu (1966)
Bendera ya Poland Poland Mshindi wa UEFA awamu ya pili 29 Machi 2022 Miaka 9 (1938, 1974, 1978, 1982, 1986, 2002, 2006, 2018, 2022) Nafasi ya tatu (1974, 1982)
Bendera ya Tunisia Tunisia Mshindi wa CAF awamu ya tatu 29 Machi 2022 Miaka 6 (1978, 1998, 2002, 2006, 2018, 2022) Hatua ya makundi (1978, 1998, 2002, 2006, 2018)
Bendera ya Moroko Moroko Mshindi wa CAF awamu ya tatu 29 Machi 2022 Miaka 6 (1970, 1986, 1994, 1998, 2018, 2022) Hatua ya mtoano ya 16 bora (1986)
Bendera ya Kamerun Cameroon Mshindi wa CAF awamu ya tatu 29 Machi 2022 Miaka 8 (1982, 1990, 1994, 1998, 2002, 2010, 2014. 2022) Robo-fainali (1990)
Marekani Nafasi ya tatu - CONCACAF awamu ya tatu 30 Machi 2022 Miaka 11 (1930, 1934, 1950, 1990, 1994, 1998, 2002, 2006, 2010, 2014, 2022) Nafasi ya tatu (1930)
Bendera ya Mexiko Meksiko CONCACAF awamu ya tatu- runners-up 30 Machi 2022 Miaka 17 (1930, 1950, 1954, 1958, 1962, 1966, 1970, 1978, 1986, 1994, 1998, 2002, 2006, 2010, 2014, 2018, 2022) Robo-fainali (1970, 1986)

Waamuzi wa michezo (marefa)

Tarehe 19 Mei 2022, FIFA ilitangaza orodha ya marefa 36, na marefa wasaidizi 69 na marefa 24 wasaidizi wa video (VAR) katika mashindano hayo.[8][9] Kati ya Waamuzi 36 FIFA ilipanga waamuzi wawili wawili kutoka katika mataifa mbalimbali yakiwemo Argentina, Brazil, Uingereza na Ufaransa. Kwa mara ya kwanza waamuzi wanawake watachezesha baadhi ya mechi katika mashindano hayo.[10][11]

Stéphanie Frappart kutoka nchini Ufaransa, Rwanda Salima Mukansanga na Yoshimi Yamashita kutoka Japani walikuwa marefa wa kike wa kwanza kuteuliwa kushiriki katika Kombe la Dunia la fifa kwa wanaume mwaka 2022 na wataungana na wanawake watatu ambao ni wasaidizi wa marefa.[12][13][14][15][16][17]

Viwanja

Mapendekezo matano ya kwanza ya Kombe la Dunia yalipendekezwa mwanzoni mwa Machi 2010. Nchi hiyo inadhamiria viwanja hivyo kuakisi masuala ya kihistoria na kiutamaduni ya Qatar, itakayozingatia vigezo na masharti yafuatayo: urithi, faraja, ufikiaji, na uendelevu.[18] Viwanja hivyo vitawekewa mfumo wa utoaji baridi ambao unalenga kupunguza joto ndani ya uwanja hadi 20 °C (36 °F), lakini bado haijafahamika kama hatua hii itafanya kazi kwenye viwanja vilivyo wazi. Miradi yote mitano ya uwanja iliyozinduliwa imeundwa na mbunifu wa nchini Ujerumani,Albert Speer na washirika wengine. Uwanja wa Al Bayt utakuwa uwanja wa pekee wa ndani wa nane kutumika.

Ripoti iliyotolewa tarehe 9 Desemba 2010 ilimnukuu Rais wa FIFA Sepp Blatter akisema kwamba mataifa mengine yanaweza kuwa mwenyeji wa mechi wakati wa Kombe la Dunia. Hata hivyo, hakuna nchi maalum zilizopewa jina kwenye ripoti hiyo. Blatter aliongeza kwa kusema kwamba uamuzi wowote lazima uchukuliwe na Qatar kwanza na kisha kupitishwa na kamati tendaji ya FIFA.[19]

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Aprili 2013 na Merrill Lynch, kitengo cha uwekezaji wa benki ya Amerika, waandaaji wa Qatar wameomba FIFA kupitisha idadi ndogo ya viwanja kwa sababu ya gharama kuongezeka.[20]

Ingawa, kufikia Aprili 2017, FIFA ilikuwa bado haijakamilisha idadi ya viwanja ambavyo Qatar ingefikia katika kipindi cha miaka mitano, Kamati Kuu ya Uwasilishaji na Urithi ya Qatar ilisema ilitarajia kuwa kutakuwa na vituo nane ndani na karibu na Doha (isipokuwa Al Khor).[21]

Mnamo Januari 2019, Infantino alisema kuwa FIFA ilikuwa inachunguza uwezekano wa kuwa na nchi jirani za mwenyeji wa mechi wakati wa mashindano, ili kupunguza mvutano wa kisiasa.[22]

Uwanja wa 974, ambao zamani ulijulikana kama Ras Abu Aboud, ni uwanja wa saba wa Kombe la Dunia la FIFA 2022 kukamilika. Jina lake linatokana na idadi ya makontena ya meli yaliyotumiwa katika ujenzi wake. Uwanja 974 utatumika kuchezea mechi saba wakati wa michuano ya kombe la dunia.[23]

Mji wa Lusail Mji wa Al Khor Mji wa Doha
Uwanja wa Michezo wa Lusail Iconic Uwanja wa Michezo wa Al Bayt ‎ Uwanja wa Michezo wa 974 Uwanja wa Michezo wa Al Thumama ‎
Uwezo: 80,000
Uwezo: 60,000 Uwezo: 40,000 Uwezo: 40,000
Mji wa Al Rayyan Mji wa Al Wakrah
Uwanja wa Michezo wa Education City Uwanja wa Michezo wa Ahmad bin Ali ‎ Uwanja wa Michezo wa Khalifa ‎ Uwanja wa Michezo wa Al Janoub
Uwezo: 45,350 Uwezo: 44,740 Uwezo: 40,000
(umeongezewa)
Uwezo: 40,000

Ratiba

Ratiba ya mechi ilithibitishwa na FIFA tarehe 15 Julai 2020.[24] Mechi pekee ya kwanza katika hatua ya makundi itachezwa siku ya ufunguzi kati ya wenyeji Qatar dhidi ya Ekuador, itachezwa tarehe 21 Novemba 2022 kwenye uwanja wa Al Bayt. Na mechi nne zitakua zikichezwa kila siku katika nyakati tofauti tofauti. Na fainali itachezwa tarehe 18 Desemba 2022 kwenye Uwanja wa Iconic wa Lusail.[25]

Matumizi ya Uwanja Kwenye Hatua ya Makundi

Kundi A, B, E na F watatumia Uwanja wa Al Bayt, Uwanja wa Kimataifa wa Khalifa, Uwanja wa Al Thumama pamoja na Uwanja wa Ahmad bin Ali.

Kundi C, D, G na H watatumia Uwanja wa Iconic wa Lusail, Uwanja wa 974, Uwanja wa Michezo wa Education City pamoja na Uwanja wa Al Janoub.

FIFA ilipanga hatua ya makundi tarehe 1 Aprili 2022.[26][27]

Matokeo ya makundi

Washindi wawili wa kila kundi wanaendelea na hatua inayofuata (rangi ya kijani kibichi).

Kundi A

Na.
Timu
Pointi Michezo Ushindi Sare Kushindwa Goli waliofunga Goli waliofungwa Tofauti ya goli
1 Bendera ya Uholanzi Uholanzi 7 3 2 1 0 5 1 4
2 Bendera ya Senegal Senegal 6 3 2 0 1 5 4 1
3 Bendera ya Jamhuri ya Dominika Jamhuri ya Dominika 4 3 1 1 1 4 3 1
4 Bendera ya Qatar Qatar 0 3 0 0 3 1 7 -6

Kundi B

Na.
Timu
Pointi Michezo Ushindi Sare Kushindwa Goli waliofunga Goli waliofungwa Tofauti ya goli.
1 Bendera ya Uingereza Uingereza 7 3 2 1 0 9 2 7
2 Marekani 5 3 1 2 0 2 1 1
3 Bendera ya Uajemi Iran 3 3 1 0 2 4 7 -3
4 Bendera ya Welisi Welisi 1 3 0 1 2 1 6 -5

Kundi C

Na.
Timu
Pointi Michezo Ushindi Sare Kushindwa Goli waliofunga Goli waliofungwa Tofauti ya goli.
1 Bendera ya Argentina Argentina 6 3 2 0 1 5 2 3
2 Bendera ya Poland Poland 4 3 1 1 1 2 2 0
3 Bendera ya Mexiko Meksiko 4 3 1 1 1 2 3 -1
4 Saudi arabia 3 3 1 0 2 3 5 -2

Kundi D

Na.
Timu
Pointi Michezo Ushindi Sare Kushindwa Goli waliofunga Goli waliofungwa Tofauti ya goli.
1 Bendera ya Ufaransa Ufaransa 6 3 2 0 1 6 3 3
2 Bendera ya Australia Australia 6 3 2 0 1 3 4 -1
3 Bendera ya Tunisia Tunisia 4 3 1 1 1 1 1 0
4 Bendera ya Denmark Denmark 1 3 0 1 2 1 3 -2

Kundi E

Na.
Timu
Pointi Michezo Ushindi Sare Kushindwa Goli waliofunga Goli waliofungwa Tofauti ya goli.
1 Bendera ya Japani Japan 6 3 2 0 1 4 3 1
2 Bendera ya Hispania Hispania 4 3 1 1 1 9 3 6
3 Bendera ya Ujerumani Ujerumani 4 3 1 1 1 6 5 1
4 Bendera ya Costa Rica Kosta Rika 3 3 1 0 2 3 11 -8

Kundi F

Na.
Timu
Pointi Michezo Ushindi Sare Kushindwa Goli waliofunga Goli waliofungwa Tofauti ya goli.
1 Bendera ya Moroko Moroko 7 3 2 1 0 4 1 3
2 Bendera ya Kroatia Kroatia 5 3 1 2 0 4 1 3
3 Bendera ya Ubelgiji Ubelgiji 4 3 1 1 1 1 2 -1
4 Bendera ya Kanada Kanada 0 3 0 0 3 2 7 -5

Kundi G

Na.
Timu
Pointi Michezo Ushindi Sare Kushindwa Goli waliofunga Goli waliofungwa Tofauti ya goli.
1 Bendera ya Brazil Brazil 6 3 2 0 1 3 1 2
2 Bendera ya Uswisi Uswisi 6 3 2 0 1 4 3 1
3 Bendera ya Kamerun Cameroon 4 3 1 1 1 4 4 0
4 Bendera ya Serbia Serbia 1 3 0 1 2 5 8 -3

Kundi H

Na.
Timu
Pointi Michezo Ushindi Sare Kushindwa Goli waliofunga Goli waliofungwa Tofauti ya goli.
1 Bendera ya Ureno Ureno 6 3 2 0 1 6 4 2
2 Bendera ya South Korea Korea Kusini 4 3 1 1 1 4 4 0
3 Bendera ya Uruguay Uruguay 4 3 1 1 1 2 2 0
4 Bendera ya Ghana Ghana 3 3 1 0 2 5 7 -2

Michezo ya ngazi za fainali mwaka 2022

Mashindano ya timu 16 Mashindano ya timu 8 Nusufainali ya timu 4 Fainali ya timu 2
                           
3 Desemba - Khalifa            
  Bendera ya Uholanzi Uholanzi   3
9 Desemba - Lusail Iconic
  Marekani   1  
  Bendera ya Uholanzi Uholanzi   2(3)
3 Desemba - Ahmad bin Ali
    Bendera ya Argentina Argentina(p)  2(4)  
  Bendera ya Argentina Argentina   2
13 Desemba - Lusail Iconic
  Bendera ya Australia Australia   1  
  Bendera ya Argentina Argentina   3
5 Desemba - Al Janoub
    Bendera ya Kroatia Kroatia  0  
  Bendera ya Japani Japan   1(1)
9 Desemba - Education City
  Bendera ya Kroatia Kroatia(p)   1(3)  
  Bendera ya Kroatia Kroatia(p)   1(4)
5 Desemba - 974
    Bendera ya Brazil Brazil  1(2)  
  Bendera ya Brazil Brazil   4
18 Desemba - Lusail Iconic
  Bendera ya South Korea Korea Kusini   1  
  Bendera ya Argentina Argentina(p)  3(4)
4 Desemba - Al Bayt ‎
    Bendera ya Ufaransa Ufaransa  3(2)
  Bendera ya Uingereza Uingereza  3
10 Desemba - Al Bayt ‎
  Bendera ya Senegal Senegal  0  
  Bendera ya Uingereza Uingereza   1
4 Desemba - Al Thumama
    Bendera ya Ufaransa Ufaransa  2  
  Bendera ya Ufaransa Ufaransa   3
14 Desemba - Al Bayt
  Bendera ya Poland Poland   1  
  Bendera ya Ufaransa Ufaransa  2
6 Desemba - Education City
    Bendera ya Moroko Moroko   0   Mshindi wa tatu
  Bendera ya Moroko Moroko(p)   0(3)
10 Desemba - Al Thumama 17 Desemba - Khalifa
  Bendera ya Hispania Hispania   0  
  Bendera ya Moroko Moroko   1   Bendera ya Kroatia Kroatia  2
6 Desemba - Lusail Iconic
    Bendera ya Ureno Ureno  0     Bendera ya Moroko Moroko  1
  Bendera ya Ureno Ureno   6
  Bendera ya Uswisi Uswisi   1  

Marejeo

  1. Elias, Jaan; Mobarak, Mushfiq; Rosenthal, Jean (2020). Qatar FIFA World Cup 2022. 1 Oliver's Yard, 55 City Road, London EC1Y 1SP United Kingdom: Yale School of Management. ISBN 978-1-5297-9640-7. 
  2. "Amir: 2022 World Cup Qatar a tournament for all Arabs", Gulf Times, 15 July 2018. 
  3. Taylor, Daniel (15 July 2018). "France seal second World Cup triumph with 4–2 win over brave Croatia". The Guardian. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 June 2019. Iliwekwa mnamo 7 September 2018.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); Check date values in: |date=, |archivedate=, |accessdate= (help)
  4. "FIFA Executive Committee confirms November/December event period for Qatar 2022". FIFA. 19 March 2015. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 10 September 2018. Iliwekwa mnamo 5 December 2017.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help); More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); Check date values in: |date=, |archivedate=, |accessdate= (help)
  5. Palmer, Dan. "Hosts Qatar to compete in qualifying for 2022 World Cup", insidethegames.biz, Dunsar Media Company, 31 July 2017. 
  6. "FIFA World Cup Qualifier: Canada joy as Jamaica rout seals first finals berth since 1986-Sports News , Firstpost". Firstpost. 28 March 2022. Iliwekwa mnamo 28 March 2022.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  7. "Italy 0–1 North Macedonia: European champions stunned in World Cup play-offs", BBC Sport, 24 March 2022. 
  8. "36 referees, 69 assistant referees and 24 video match officials appointed for FIFA World Cup Qatar 2022". FIFA. 19 May 2022. Iliwekwa mnamo 19 May 2022.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  9. "FIFA World Cup Qatar 2022 – List of appointed FIFA Match Officials". FIFA. 19 May 2022. Iliwekwa mnamo 19 May 2022.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  10. "Qatar World Cup: Women referees to feature for first time in men's competition". ESPN. 20 May 2022. Iliwekwa mnamo 20 May 2022.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  11. "Frappart: Final role a huge source of pride". 
  12. "Bakary Gassama". 
  13. "Juan Pablo Belatti". 
  14. "World Cup 2018 Russia". 
  15. "César Ramos Palazuelos". 
  16. "Janny Sikazwe". 
  17. "Alireza Faghani". 
  18. Hayajneh, Abdelnaser; Elbarrawy, Hassan; El Shazly, Yassin; Rashid, Tarek (December 2017). "Football and Sustainability in the Desert, Qatar 2022 Green World Cup's Stadiums: Legal Perspective". European Journal of Social Sciences: 475–493. SSRN 3096185.  Check date values in: |date= (help)
  19. "Report: Qatar neighbors could host 2022 WC games", Fox Soccer/AP, 9 December 2010. 
  20. "Qatar 2022: Nine stadiums instead of twelve? –". Stadiumdb.com. 25 April 2013. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 October 2013. Iliwekwa mnamo 25 May 2013.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); Check date values in: |date=, |archivedate=, |accessdate= (help)
  21. "Stadiums". Supreme Committee for Delivery & Legacy. 6 July 2018. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 14 November 2017. Iliwekwa mnamo 8 January 2018.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help); More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); Check date values in: |date=, |archivedate=, |accessdate= (help)
  22. "Infantino: Qatar neighbours could help host World Cup". ESPN. 2 January 2019. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2 January 2019. Iliwekwa mnamo 2 January 2019.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); Check date values in: |date=, |archivedate=, |accessdate= (help)
  23. Welle (www.dw.com), Deutsche, Qatar touts dismountable stadium for 'sustainable' 2022 World Cup | DW | 25 November 2021, iliwekwa mnamo 30 November 2021  Check date values in: |accessdate= (help)
  24. "FIFA World Cup match schedule confirmed: hosts Qatar to kick off 2022 tournament at Al Bayt Stadium". FIFA.com. 15 July 2020. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 December 2020. Iliwekwa mnamo 15 July 2020.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); Check date values in: |date=, |archivedate=, |accessdate= (help)
  25. "FIFA World Cup Qatar 2022 Match Schedule". FIFA.com. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 15 July 2020. Iliwekwa mnamo 15 July 2020.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)
  26. "Final match schedule for the FIFA World Cup Qatar 2022 now available". FIFA. 1 April 2022. Iliwekwa mnamo 1 April 2022.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  27. "FIFA World Cup Qatar 2022 – Match Schedule". FIFA. 1 April 2022. Iliwekwa mnamo 1 April 2022.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Kombe la Dunia la FIFA 2022 kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.