Nenda kwa yaliyomo

Uwanja wa Michezo wa Al Bayt

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uwanja wa Michezo wa Al Bayt

Uwanja wa Michezo wa Al Bayt (kwa Kiarabu: استاد البيت) Ni uwanja wa mpira wa miguu uliyopo ndani ya mji wa Al Khor nchini Qatar. Ni uwanja ambao utatumika katika mashindano ya Kombe la Dunia la FIFA LA mwaka 2022 kuanzia[1] tarehe 21 Novemba 2022 hadi 18 Desemba 2022.[2] Mkataba wa ujenzi wa uwanja huu walipewa Webuild S.p.A na Cimolai mwaka 2015.[3][4]

Uwanja huu upo takriban kilomita 35 kutoka Doha[5].

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Uzinduzi wa uwanja ulifanyika tarehe 30 Novemba 2021, wakati wa sherehe za ufunguzi wa 2021 wa Kombe la Waarabu la FIFA (FIFA Arab Cup 2021). Baada ya mechi kati ya mwenyeji Timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Qatar na timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Bahrain na mechi kumalizika kwa goli 1:0 goli likifungwa kwa kichwa na Abdulaziz Hatem katika dakika ya 69 ya mchezo huo.[6]

Hafla hii ilihudhuriwa na Amiri (mkuu wa nchi) ya Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, Rais wa FIFA Gianni Infantino, wakuu kadhaa wa nchi na mamlaka na marais kutoka vyama wanachama kufurahia sherehe za uzinduzi wa Uwanja wa Al Bayt na kuadhimisha ufunguzi rasmi wa kombe la fifa la Uarabuni 2021. Uwanja wa Al Bayt ulijengwa na kuchezewa mechi tano pamoja na mchezo wa fainali uliyochezwa tarehe 18 Desemba 2021 wakati wa Kombe la fifa la nchi za kiarabu mwaka 2021 .

  1. Neha Bhatia (13 Agosti 2015). "Revealed: The firms behind the construction Qatar's World Cup stadiums". Arabian Business. Iliwekwa mnamo 13 Agosti 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Al Bayt Stadium: All you need to know about Qatar's new 2022 World Cup venue". goal.com. 1 Desemba 2021. Iliwekwa mnamo 2 Machi 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Salini Cimolai JV - News". 
  4. "Education City Stadium awarded prestigious sustainability certificates". FIFA. 16 Januari 2020. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Januari 2020. Iliwekwa mnamo 18 Mei 2020. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Eggeling, Kristin Anabel (2020). Nation-branding in practice : the politics of promoting sports, cities and universities in Kazakhstan and Qatar. Abingdon, Oxon. ISBN 978-0-367-82157-9. OCLC 1142893503.{{cite book}}: CS1 maint: location missing publisher (link)
  6. "Algeria win the FIFA Arab Cup". fifa.com. 18 Desemba 2021. Iliwekwa mnamo 7 Machi 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa Michezo wa Al Bayt kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.