Nenda kwa yaliyomo

Refa msaidizi wa video

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mwamuzi akiangalia yaliyojiri kwenye mechi.

Refa msaidizi wa video (kwa Kiingereza: Video assistant referee; kifupi: VAR) ni msaidizi wa refa katika michezo ya mpira wa miguu ambao humuonesha mwamuzi kilichotokea katika tukio la mchezo kwa kutumia kumbukumbu ya video. Mnamo mwaka wa 2018, VAR ziliandikwa kwenye Sheria za mchezo na bodi ya Kimataifa ya Chama cha Soka (IFAB).

Kuna aina 4 za wito ambazo zinaweza kupitiwa na VAR. 1. Magoli ikiwa kulikuwa na ukiukwaji wa sheria wakati wa awamu ya kushambulia, kama vile faulo na Offside. 2. Maamuzi ya penati (pengine si sahihi) 3. Maamuzi ya moja kwa moja ya kadi nyekundu (kadi ya pili ya njano haipatikani) 4. Uthibitisho uliopo katika kutoa kadi nyekundu au ya njano.

VAR imetumika katika fainali za kombe la Dunia nchini Urusi. Na sasa hata katika ligi kuu za Uingereza, Hispania, Ufaransa, Italia, Ujerumani n.k.

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Refa msaidizi wa video kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.