Uwanja wa Michezo wa Ahmad bin Ali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uwanja wa michezo wa Ahmad bin Ali

Uwanja wa michezo wa Ahmad bin Ali (kwa Kiarabu: ملعب أحمد بن علي; maarufu kama uwanja wa Al-Rayyan) ni uwanja wenye matumizi mbalimbali huko Al Rayyan, nchini Qatar, Kwa sasa unatumiwa zaidi kwa mechi za mpira wa miguu. Ni uwanja wa nyumbani wa klabu ya Al-Rayyan na Al-Khaitiyath. Uwanja huu wa michezo ulipewa jina la Ahmad bin Ali Al Thani, Amiri wa Qatar kuanzia mwaka 1960 hadi 1972.[1][2]

Uwanja huu wa zamani, ulijengwa mwaka 2003, ulikuwa na uwezo wa kuchukua watu 21,282 na ulibomolewa mwaka 2015. [3]Uwanja mpya wa Al Rayyan una uwezo wa kubeba watu 40,740. Ni uwanja utakao tumika kwenye michuano ya kombe la dunia la FIFA 2022.


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa Michezo wa Ahmad bin Ali kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.