Farasi (kundinyota)
Kwa habari kuhusu mnyama angalia Farasi
Farasi (Pegasus kwa Kilatini na Kiingereza) [1] ni jina la kundinyota kubwa kwenye nusutufe ya kaskazini ya Dunia.
Mahali pake
Farasi linapakana na makundinyota jirani ya Mara ( Andromeda), Mjusi ( Lacerta), Dajaja ( Cygnus), Mbweha (Vulpecula), Dalufnin (Delphinus), Kifarasi (Equuleus), Dalu (Aquarius), Hutu ( Pisces)
Jina
Jina la Farasi linatokana na Kiarabu الفرس al-faras ambalo ni umbo la jina asilia la Kigiriki Ίππος hippos yaani farasi. Baadaye ilikuwa Πήγασος au Pegasus kwa tahajia ya Kilatini. Wagiriki wa Kale walitumia jina hili kwa kutaja farasi mwenye mabawa katika mitholojia yao.
Pegasus - Farasi ni kati ya makundinyota yaliyotajwa tayari na Klaudio Ptolemaio katika karne ya 2 BK. Lipo pia katika orodha ya makundinyota 88 ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia kwa jina la Pegasus. Kifupi chake rasmi kufuatana na UKIA ni 'Peg'. [2]
Nyota
Nyota tatu za Alfa, Beta na Gamma Pegasi pamoja na Alpheratz (Alfa Andromedae) zinafanya pembenne.
Nyota angavu zaidi ni au Epsilon Pegasi au Enif (ar. أنف anif kwa maana « pua ») yenye mwangaza unaoonekana wa mag 2.38[3]. Ni nyotajitu yenye umbali wa miakanuru 670 kutoka Duniani. [4]
Jina la (Bayer) |
Namba ya Flamsteed |
Jina (Ukia) |
Mwangaza unaoonekana |
Umbali (miaka nuru) |
Aina ya spektra |
---|---|---|---|---|---|
ε Epsilon | 8 | Anufu ya Farasi (Enif) | mag 2,39 | 673 | K2 Ib |
β Beta | 53 | Scheat | mag 2,4 - 3,0 | 199 | M222 II-III |
α Alfa | 54 | Marikabu (Markab) | mag 2,49 | 140 | B9.5 III |
γ Gamma | 88 | Algenib | mag 2,80 - 2,86 | 333 | B2 IV |
η Eta | 44 | Matar | mag 2,93 | 215 | G2 II-III |
ζ Dzeta | 42 | Homam | mag 3,41 | 209 | B8.5 V |
μ Mu | 48 | Sadalbari | mag 3,51 | 117 | M2 III |
θ Theta | 26 | Biham | mag 3,52 | 97 | A2V |
ι Iota | 24 | mag 3,77 | 38 | F5 V | |
λ Lambda | 47 | mag 3,97 | 395 | G8 II-III |
Tanbihi
- ↑ Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Pegasus" katika lugha ya Kilatini ni " Pegasi " na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Pegasi, nk.
- ↑ The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Oktoba 2017
- ↑ Naming stars, tovuti ya UKIA, iliangaliwa Oktoba 2017
- ↑ ENIF (Epsilon Pegasi), tovuti ya Prof Jim Kaler, University of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017
Viungo vya Nje
- Constellation Guide: Pegasus constellation
- Pegasus , « Stars », kwenye tovuti ya Prof Jim Kaler, University of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017
- Star Tales – Pegasus
- The Deep Photographic Guide to the Constellations: Pegasus
Marejeo
- Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, “Pegasus” ukurasa 321 ff (online hapa kwenye archive.org)