Anufu ya Farasi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Anufu ya Farasi
(Epsilon Pegasi, Enif)
Kundinyota Farasi (Pegasus)
Mwangaza unaonekana 2.4
Kundi la spektra K2 I
Paralaksi (mas) 4.73 ± 0.17
Umbali (miakanuru) 690
Mwangaza halisi 4.14
Masi M☉ 11.7
Nusukipenyo R☉ 185
Mng’aro L☉ 3895
Jotoridi usoni wa nyota (K) 4279
Majina mbadala Enf, Enir, Al Anf, Os Pegasi, 8 Peg, BD+09° 4891, FK5 815, HD 206778, HIP 107315, HR 8308, SAO 127029


Anufu ya Farasi (lat. & ing. Enif pia ε Epsilon Pegasi [1], kifupi Epsilon Peg’’’, ε Peg’’’) ni nyota angavu zaidi katika kundinyota la Farasi (Pegasus).

Jina

Anufu ya Farasi inayomaanisha “Pua la Farasi” ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. [2]. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wanaosema kwa kawaida الأنف al-anfu inayomaanisha "pua"..

Kwa matumizi ya kimataifa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia ulikubali jina la Kiarabu na kuorodhesha nyota kwa jina la "Enif" [3] .

Epsilon Pegasi ni jina la Bayer ; ingawa Epsilon ni herufi ya tano katika Alfabeti ya Kigiriki na Anufu ya Farasi ni nyota angavu zaidi katika Farasi - Pegasus. Bayer alifuata hapa tena utaratibu jinsi gani nyota angavu zinaonekana angani akatangulia kutaja nyota angavu za pembenne ya Farasi.

Tabia

Anufu ya Farasi ni nyota jitu jekundu katika kundi la spektra K2 ikiwa umbali wa karibu miaka nuru 700. Baada ya miaka milioni kadhaa itakwisha kama nyota kibete cheupe. Inawezekana pia ya kwamba italipuka kama nyota nova.

Anufu ya Farasi ni nyota badilifu isiyofuata utaratibu maalumu iliyotambuliwa katika mageuko yake. Wakati mwingine inarusha masi kubwa nje yake na hapo mwangaza wake unaongezeka. Mwaka 1972 ilitazamiwa kuongeza mng’aro kwa muda wa dakika 10 hadi kufikia mwangaza sawa na nyota ya Tairi wa mara tano kawaida yake.[4]

Tanbihi

  1. Pegasi ni uhusika milikishi (en:genitive) wa "Pegasus" katika lugha ya Kilatini na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa, Beta, Epsilon Pegasi, nk.
  2. ling. Knappert 1993
  3. Naming Stars, tovuti ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia (Ukia), iliangaliwa Novemba 2017
  4. Jim Kaler, ENIF (Epsilon Pegasi)

Viungo vya Nje

Marejeo

  • Allen, Richard Hinckley: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 331 (online kwenye archive.org)
  • Knappert, Jan: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331
  • Enif katika Bright Star Catalogue online hapa
  • Smith, Verne V.; Lambert, David L. (June 1987), "Are the red supergiants Epsilon Peg and 12 PUP victims of mild s-processing?", Monthly Notices of the Royal Astronomical Society, 226 (3): 563–579