Nenda kwa yaliyomo

Bikira Maria wa Lurdi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Bikira Maria wa Lourdes)
Bikira Maria akitokea Lourdes akiwa na rosari. Maneno yaliyoandikwa ni ya Kifaransa: Je suis l'Immaculée conception (Ndimi Kukingiwa Dhambi Asili), miaka 4 baada ya Papa Pius IX kutangaza dogma ya Maria Kukingiwa dhambi ya asili.[1]

Bikira Maria wa Lurdi (kwa Kifaransa: Notre Dame de Lourdes au Notre-Dame-de-Lourdes; kwa Kiingereza "Our Lady of Lourdes") ni jina mojawapo la Bikira Maria lililotokana na njozi maarufu zilizojirudia mwaka 1858 alizozisimulia Bernadeta Soubirous, msichana mnyenyekevu wa Lourdes, Ufaransa.

Binti huyo alisema kwamba aliwezeshwa kumuona mara kadhaa katika pango la Massabielle kati ya milima Pirenei kwenye mto Gave karibu na kijiji cha Lourdes [2].

Njozi hizo zilithibitishwa na Kanisa Katoliki kuwa za kuaminika, hata ikaanzishwa kumbukumbu yake katika liturujia kila tarehe 11 Februari, ilipotokea njozi ya kwanza[3]. Kutokana na wingi wa miujiza iliyowatokea wagonjwa wanaohiji huko kwa mamilioni, siku hiyo inaadhimishwa na Kanisa kama Siku ya Kimataifa ya Wagonjwa.

Marejeo ya Kiswahili

[hariri | hariri chanzo]
  • Masomo ya Breviari - Sikukuu za Bwana, za Bikira Maria na za Watakatifu - Ndanda Mission Press 1978, uk 62-64
  • John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 51-52
  • Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 43-44

Marejeo ya lugha nyingine

[hariri | hariri chanzo]
  • Harris, Ruth (1999). Lourdes: Body and Spirit in the Secular Age. Penguin Books. ISBN 0-71-399186-0.
  • Lasserre, Henri (1906). Our Lady of Lourdes (tol. la 11th). New York: P. J. Kenedy & Sons.
  • Laurentin, L. (1988). "Lourdes". Marienlexikon. Regensburg: Eos Verlag.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bikira Maria wa Lurdi kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.