Ukulu mtakatifu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Holy See)
Jump to navigation Jump to search
Ukulu wa Papa ndani ya Kanisa kuu la Roma, yaani Basilika la Mt. Yohane huko Laterani, ni ishara ya Ukulu mtakatifu.
Hii ni sehemu ya mfululizo kuhusu
Kanisa Katoliki
StPetersBasilicaEarlyMorning.jpg
Imani

Umoja wa Mungu
Utatu (Baba, Mwana, Roho Mtakatifu)
Umwilisho Maisha ya Yesu
Msalaba Ufufuko Kupaa
Historia ya Wokovu Ufunuo
Biblia Mapokeo Ualimu Dogma
Neema Dhambi Wokovu Sakramenti
Watakatifu Bikira Maria

Muundo

Papa: Fransisko
Urika wa maaskofu Mitaguso mikuu
Kundi la Makardinali
Kanisa la Kilatini
Makanisa Katoliki ya Mashariki

Historia

Historia Ukristo
Ukatoliki Mlolongo wa Kitume
Sifa nne za Kanisa Utetezi Ekumeni
Maisha ya kiroho Amri Kumi Utawa
Sala Falsafa Teolojia
Muziki Sanaa Sayansi

Ibada

Liturujia Mwaka wa Kanisa
Ekaristi Liturujia ya Vipindi

Mapokeo ya liturujia

Liturujia ya Kilatini (Roma Trento Milano Toledo Braga Lyon Canterbury)
Liturujia ya Armenia Liturujia ya Misri
Liturujia ya Ugiriki Liturujia ya Antiokia
Liturujia ya Mesopotamia

Ukulu mtakatifu au Ukulu wa Kitume ni hasa kiti maalumu alichowekewa Papa katika Kanisa kuu la Roma, ambacho ni ishara ya mamlaka ya kiaskofu ambayo Wakatoliki wanasadiki anayo ya kufundisha, kutakasa na kuongoza Taifa la Mungu kokote duniani.

Katika imani ya Kikatoliki[hariri | hariri chanzo]

Kwa msingi huo, ukulu unamwakilisha Papa kama kiongozi wa Kanisa Katoliki lote duniani na kuhusiana na dogma ya kwamba ana karama ya kutodanganyika anapofundisha "rasmi" (kwa Kilatini "ex cathedra", yaani "kutoka ukulu") kama mkuu wa kundi la maaskofu.

Katika liturujia[hariri | hariri chanzo]

Sikukuu ya ukulu huo inaadhimisha kila mwaka tarehe 22 Februari kwa jina la Ukulu wa Mtume Petro, anayeaminiwa kuwa ndiye aliyewarithisha Mapapa mamlaka yake kama mkuu wa Mitume wa Yesu.

Katika sheria za Kanisa[hariri | hariri chanzo]

Kadiri ya Mkusanyo wa Sheria za Kanisa la Kilatini (kanuni 361), "Ukulu mtakatifu" ni jina rasmi linalotumika kuwamaanisha Papa na miundo yote inayomsaidia kuongoza Kanisa Katoliki duniani ikiwa na makao makuu mjini Roma.

Ukulu usipokuwa na Papa[hariri | hariri chanzo]

Wakati Kanisa linapobaki halina Papa (kutokana na kifo au kujiuzulu), uongozi wake unashikwa na Kundi la Makardinali ambalo pia lina wajibu na haki ya kumchagua mwandamizi wake.

Katika mafungamano ya kimataifa[hariri | hariri chanzo]

Nchi zenye uhusiano na Ukulu mtakatifu.      Uhusiano wa kibalozi      Uhusiano mwingine      Bila uhusiano rasmi

Ukulu mtakatifu una hadhi ya nafsi ya kisheria katika sheria za kimataifa kutokana na umbile lake, mapokeo ya historia na mahitaji ya utume wake.

Ukulu mtakatifu unawakilisha kwa pamoja Kanisa Katoliki na nchi huru ya Mji wa Vatikani (ambayo iko chini ya mamlaka yake) katika mafungamano ya kimataifa na nchi yoyote duniani na miundo ya kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa, ambapo unatambulika kama mojawapo kati ya watazamaji wa kudumu.

Ukulu mtakatifu na Vatikani[hariri | hariri chanzo]

Kisheria, Ukulu mtakatifu ni tofauti na Mji wa Vatikani ambayo ni nchi huru inayotawaliwa na Papa.

Eneo dogo la nchi hiyo (kilometa mraba 0.44) linadaiwa na kutosha ili kuhakikisha uhuru wa miundo ya Kanisa katika kutekeleza majukumu yake.

Mabalozi wanaowakilisha nchi huru nyingine (180, mwanzoni mwa mwaka 2013) wanatumwa kwa Ukulu mtakatifu, si kwa nchi ya Vatikani.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: