Nenda kwa yaliyomo

Tarso

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Tarsus)
Mskiti na mnara wa Küçük huko Tarso.

Tarso (kwa Kituruki na Kilatini: Tarsus; Kigiriki: Ταρσός) ni mji wa kale na wilaya iliopo katika Mkoa wa Mersin kwenye Kanda ya Mediteranea kusini mwa Uturuki.

Iko mdomoni wa mto Tarsus Cay (jina la kale: Kydnos) karibu na mwambao wa Mediteranea.

Mji una wakazi 216,382 (sensa ya mwaka 2000).

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Mji ulianzishwa tayari katika milenia ya nne KK.

Tarso ilikuwa na majina mbalimbali katika historia yake kama vile Antiokia kwenye Kydnos au Juliopolis.

Tangu karne ya 1 KK mji ulikuwa chini ya Dola la Roma. Wakazi wake wote (pamoja na Wayahudi wa mji) walipewa uraia wa Roma.

Mji wa Mtume Paulo

[hariri | hariri chanzo]

Tarso au Tarsus imejulikana zaidi kama mji alikozaliwa mtume wa Ukristo Paulo wa Tarso. Ndivyo Paulo alivyopata kuwa Mroma ingawa alifika Roma kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 54 hivi.

Makala hii kuhusu maeneo ya Uturuki bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tarso kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.