Tarso

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Tarso (Kituruki na Kilatini: Tarsus; Kigiriki: Ταρσός) ni mji wa kale katika wilaya ya Mersin ya Uturuki ya Kusini.

Iko mdomoni wa mto Tarsus Cay (jina la kale: Kydnos) karibu na mwambao wa Mediteranea.

Mji ulianzishwa tayari katika milenia ya nne KK.

Tarso ilikuwa na majina mbalimbali katika historia yake kama vile Antiokia kwa Kydnos au Juliopolis.

Mji una wakazi 216,382 (sensa ya mwaka 2000).

Mji wa Mtume Paulo[hariri | hariri chanzo]

Tarso au Tarsus imejulikana zaidi kama mji alikozaliwa mtume wa Ukristo Paulo wa Tarso. Tangu karne ya 1 KK mji ulikuwa chini ya Dola la Roma. Wakazi wake wote (pamoja na Wayahudi wa mji) walipewa uraia wa Kiroma. Hivyo Paulo alikuwa raia Mroma.

Turkey stub.png Makala hii kuhusu maeneo ya Uturuki bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tarso kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.