Thug Life: Volume 1

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Thug Life: Volume 1
Thug Life: Volume 1 Cover
Studio album ya Tupac na Thug Life
Imetolewa 26 Septemba 1994
Imerekodiwa 1993-1994
Aina G-Funk, West Coast hip hop
Urefu 42:28
Lebo Interscope/Atlantic Records (First pressing)
Amaru/BMG/Jive Records (Second pressing)
Mtayarishaji Nate Dogg, Easy Mo Bee, Warren G, Johnny "J", Mopreme, Syke
Tahakiki za kitaalamu
Wendo wa albamu za Tupac na Thug Life
Strictly 4 My N.I.G.G.A.Z.
(1993)
Thug Life: Volume 1
(1994)
Me Against the World
(1995)
Single za kutoka katika albamu ya Thug Life: Volume 1
  1. "Pour Out a Little Liquor"
    Imetolewa: 23 Agosti 1994
  2. "Cradle to the Grave"
    Imetolewa: 17 Januari 1995

Thug Life: Volume 1 ilikuwa albamu ya kwanza kutolewa na kundi la Thug Life, lililoanzishwa na rapa Tupac Shakur, na ilitolewa mnamo tar. 26 Septemba 1994. Awali albamu ilitolewa na studio ya Shakur ya Out Da Gutta Records. Kwa kufuatia upondaji mkubwa juu ya muziki wa gangsta rap kwa kipindi hicho, toleo halisi la albamu likatiwa kapuni na kurekodiwa upya na nyimbo nyingine mpya kibao na zile baadhi za awali kukatwa. Ilisemekana kwamba 2Pac alitengeneza matoleo mengine mawili ya albamu hii, yenye nyimbo kibao ambazo bado hazikutolewa. Kundi linaunganishwa na Big Syke, Macadoshis, Mopreme, The Rated R na Tupac Shakur. Miongoni mwa nyimbo kali kutoka kwenye albamu hii ni pamoja na "Bury Me a G","Cradle to the Grave", "Pour Out a Little Liquor", "How Long Will They Mourn Me?" na "Str8 Ballin". Mnamo mwaka wa 1996 Big Syke na Shakur walipanga watengeneze toleo la pili la Thug Life: Vol. 2 - Out On Bail ambayo ilitakiwa itolewe na studio ya Makaveli Records, lakini yale mauaji ya mwisho ya mjini Las Vegas yamesababisha hili lisiwe kweli[1]. Japokuwa awali albamu ilitolewa chini ya studio ya Shakur ya Out Da Gutta, Amaru Entertainment, studio ambayo inamilikiwa na mama yake Tupac Shakur, imekuwa ikipata haki zake. Thug Life: Volume 1 ilitunukiwa Dhahabu[2]

Orodha ya Nyimbo[hariri | hariri chanzo]

# Jina Mwimbaji Mtayarishaji
1 "Bury Me a G" 2Pac, Mopreme, Rated R, Big

Syke, Macadoshis, Natasha Walker na Stretch

Thug Music
2 "Don't Get It Twisted" Mopreme, Macadoshis na Rated R Jay na Mopreme
3 "Shit Don't Stop" 2Pac, Macadoshis, Rated R,

Mopreme, Big Syke na Y.N.V.

Thug Music
4 "Pour Out a Little Liquor" 2Pac Johnny "J"
5 "Stay True" 2Pac, Stretch na Mopreme Thug Music
6 "How Long Will They Mourn Me?" 2Pac, Nate Dogg, Big

Syke, Rated R na Macadoshis

Nate Dogg na Warren G
7 "Under Pressure" 2Pac na Stretch Thug Music
8 "Street Fame" 2Pac, Mopreme, Big Syke na Rated R Stretch
9 "Cradle to the Grave" 2Pac, Mopreme, Rated R,

Macadoshis na Big Syke

Jay Choi na Big Syke
10 "Str8 Ballin" 2Pac Easy Mo Bee

Nafasi ya Chati ya Albamu[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Albamu Nafasi za Chati
Billboard 200 Top Hip Hop Albums
1994 Thug Life Vol. 1 #42 #6

Nafasi za Chati za Single[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Wimbo Nafasi ya Chati
The Billboard Hot 100 Hot R&B/Hip-Hop Singles & Tracks Hot Rap Singles
1995 "Cradle to the Grave" - #91 #25

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. http://www.donkilluminati.com/interviews.htm Archived 17 Mei 2010 at the Wayback Machine. Exclusive Big Syke Interview
  2. [1] Archived 4 Septemba 2015 at the Wayback Machine.Riaa Searchable Database Thug Life

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]


Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Thug Life: Volume 1 kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.