Runnin' (From tha Police)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
"Runnin' (From Tha Police)"
Wimbo wa 2Pac akishirikiana na The Notorious B.I.G., Dramacydal, Stretch, na Buju Banton
Aina ya wimbo Hip hop ya kisiasa, Gangsta Rap
Urefu 3:45
Studio Black Jam
Mtunzi Tupac Shakur, Christopher Wallace
Mtayarishaji Easy Mo Bee

Runnin' (From Tha Police) ni wimbo wa 1995 ulioimbwa na rapa Tupac Shakur, akishirikiana na The Notorious B.I.G., Stretch, Dramacydal na Buju Banton. Wimbo huu huoenekana kama muhimu kwa sababu ni moja kati ya nyimbo zilizofanywa pamoja baina ya 2Pac na The Notorious B.I.G. kabla ya kuja kuwa maadui hapo baadaye, ambapo ilipelekea kuto-rekodi nyimbo pamoja tena hadi kufa kwao.

Mstari wa kwanza unaimbwa na mtu wa tatu katika kundi la watu nne Dramacydal ambaye baadaye kaenda kujiunga na kundi la 2Pac la Outlawz (Yaki Kadafi, Kastro, na E.D.I. Amin), ya pili imeimbwa na Stretch na The Notorious B.I.G., na ya tatu na ya mwisho imeimbwa na 2Pac, huku Buju Banton akiimba kiitikio.

Wasanii wanne wa katika wimbo huu wameuawa, 2Pac, Biggie, Yaki Kadafi, na Stretch.

Orodha ya nyimbo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Runnin' (From tha Police)" (Stone's Radio RMX)
  2. "Runnin' (From tha Police)" (Stone's RMX Full Length)
  3. "Runnin' (From tha Police)" (Stone's Original Vibe Mix)
  4. "Runnin' (From tha Police)" (RMX Full TV Track)
  5. "Runnin' (From tha Police)" (RMX Full Instrumental)