Untouchable

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“Untouchable (Swizz Beatz Remix)”
“Untouchable (Swizz Beatz Remix)” cover
Single ya 2Pac akishirikiana na Bone Thugs-N-Harmony
kutoka katika albamu ya Pac's Life
Imetolewa 2006
Muundo CD, Vinyl
Aina Gangsta rap
Urefu 3:53
Studio Amaru/Interscope
Mtunzi Tupac Shakur
Mtayarishaji Swizz Beatz
Mwenendo wa single za 2Pac akishirikiana na Bone Thugs-N-Harmony
"Ghetto Gospel"
(2005)
"Untouchable"
(2006)
"Pac's Life"
(2006)

"Untouchable" ni single iliyotolewa baada ya kufa kwa msanii wa muziki wa hip hop Tupac Shakur. Wimbo umemshirikisha msanii mwingine Krayzie Bone. Wimbo unatoka katika albamu ya Pac's Life. Wimbo ulitengenezewa reamixi yake na Swizz Beatz, ulikuwa wimbo wa pili wa kitaa kutolewa nyuma ya wimbo Pac's Life. Wimbo uliingia na kushika nafasi ya #91 kwenye chati za Hot R&B/Hip-Hop Singles & Tracks na #21 kwenye chati za Hot R&B/Hip-Hop Singles -ulioanza kuuzwa mnamo tar. 2 Desemba 2006 toleo la jarida la Billboard. Mstari wa Tupac una mashairi sawa na yale ya kutoka katika nyimbo zingine kama vile Drunk freestyle, Killuminati na wimbo usiotolewa wa War Games. Nyimbo hizi zote zina mashairi sawa kwa sababu Tupac hakunuia kuzitoa au nyimbo za namna hii ziwe wazi. Mara kwa mara Tupac alikuwa akitumia nyimbo zisizotolewa kuwasawazisha mashairi yake ya sasa yawe vyema.