Keep Ya Head Up

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“Keep Ya Head Up”
“Keep Ya Head Up” cover
Single ya Tupac Shakur
kutoka katika albamu ya Strictly 4 My N.I.G.G.A.Z.
B-side I Wonder If Heaven Got a Ghetto
Imetolewa 28 Oktoba 1993
Muundo 12" single
Imerekodiwa 1992
Aina Hip hop
Urefu 4:22
Studio Interscope
Mtunzi Tupac Shakur
Mtayarishaji DJ Daryl
Certification Gold (RIAA)
Mwenendo wa single za Tupac Shakur
"I Get Around"
(1993)
"Keep Ya Head Up"
(1993)
"Papa'z Song"
(1993)

"Keep Ya Head Up" ni jina la kutaja kibao kikali cha mwaka wa 1993, ambacho kilitolewa na msanii wa muziki wa hip hop Tupac Shakur. Kina gusia hasa masuala yanayohusiana na ukosefu wa nidhamu kwa jinsia ya kike, hasa kwa wale wakina-mama maskini - weusi. Kibao kina ujumbe maridhawa na mara kwa mara hutumiwa kama mfano wa upande mwepesi au laini wa Shakur.

Wengi huhesabia moja kati ya nyimbo za rap za huzuni ambazo hazijawahi kutengenezwa na mara kwa mara hutujwa na wasanii wengine kwenye kazi zao, inajenga utu wa Shakur kama rapa mwenye kujitambua na mwenye athira kubwa ya muziki wa rap, amepigiwa kura #11 kwenye 100 Bora ya Nyimbo za Rap za About.com, pamoja na "Dear Mama" imepigiwa kura nafasi ya #4.[1]

Ilitolewa kwa mara ya kwanza mnamo 1993 kutoka katika albamu ya Shakur' ya Strictly 4 My N.I.G.G.A.Z., baadaye imeonekana baada ya kifo chake mnamo 1998 kwenye kompilesheni ya albamu yake ya Vibao Vikali. Baadaye ikafuatiwa na wimbo wa Baby Don't Cry (Keep Ya Head Up II) ukiwa kama sehemu ya pili ya kibao hiki - hapo mnamo 1999 na kibao hicho kilitolewa kwenye albamu ya 2Pac ya Still I Rise.

Biti la wimbo huu limechukua sampuli ya wimbo wa Zapp & Roger wa "Be Alright" na kiitikio chake kimechukua sampuli ya wimbo wa The Five Stairsteps' "O-o-h Child", lakini hapo awali ulichukua sampuli ya Big Daddy Kane ya "Prince of Darkness". Kibao kimechukua nafasi ya #2 kwenye chati za Rap nchini Marekani, #7 kwenye chati za Hip Hop/R&B na #12 kwenye chati za Billboard Hot 100.

Orodha ya nyimbo[hariri | hariri chanzo]

CDS - maxi single

  1. "Keep Ya Head Up" (LP Version)
  2. "Keep Ya Head Up" (Vibe Tribe Remix)
  3. "Keep Ya Head Up" (Madukey Remix)
  4. "Rebel of the Underground"
  5. "I Wonder If Heaven Got a Ghetto"

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Top 100 Rap Songs". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-08-27. Iliwekwa mnamo 2010-05-06.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]