Yaki Kadafi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Yaki Kadafi
Kadafi mnamo 1995
Taarifa za awali
Jina la kuzaliwaYafeu Akiyele Fula
Pia anajulikana kamaYoung Hollywood, Felony, Killa Kadafi, The Prince
Amezaliwa(1977-10-09)Oktoba 9, 1977
The Bronx, New York, U.S.
Amekufa10 Novemba 1996 (umri 19)
Orange, New Jersey, U.S.
Miaka ya kazi1994–1996
StudioHavenotz, Cold Flo, 1 Nation
Ameshirikiana na2Pac, Hussein Fatal, Outlawz, Tha Dogg Pound, Nate Dogg, O.F.T.B., Snoop Dogg, Boot Camp Clik

Yafeu Akiyele Fula (alijulikana zaidi kwa jina lake la kisanii kama Yaki Kadafi; 9 Oktoba 197710 Novemba 1996) alikuwa rapa kutoka nchini Marekani na mwanachama mwanzilishi wa vikundi vya hip hop Outlawz na Dramacydal.

Maisha ya awali na elimu[hariri | hariri chanzo]

Yafeu Fula alizaliwa mjini Bronx, New York City mnamo Oktoba 9, 1977 na Sekou Odinga na Yaasmyn Fula. Alipokuwa na umri wa miaka minne, baba yake, Odinga, alikamatwa na kushtakiwa kwa makosa sita ya jaribio la mauaji, vitendo tisa vya kupanga njama za udanganyifu, kusaidia kumtorosha Assata Shakur kutoka gerezani na wizi mkali wa lori la silaha. Yafeu alilelewa na mama yake, ambaye jina la wazazi wake aliliasili. [1]

Wazazi wa Kadafi wote walikuwa wanachama wa chama cha Black Panther. [2] Yaasmyn Fula na mama wa Tupac Shakur, Afeni Shakur, walikuwa marafiki wa karibu, na Kadafi na Tupac waliendelea kuwa marafiki mpaka kifo chao mnamo 1996.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 1994, Fula alimkimbilia rafiki yake wa utotoni Mutah "Napoleon" Beale. Mama ya Yafeu akamtambulisha Napoleon kwa Tupac Shakur, na wote watatu wakaunda kundi la Dramacydal. Yafeu, wakati huo akiwa na miaka16 tu, alichagua jina la kisanii kaa "Young Hollywood." Kikundi hicho kilionekana kwenye albamu ya Tupac ya Me Against the World .

Wakati Tupac akiwa gerezani mnamo wa 1995 kwa mashtaka ya unyanyasaji wa kijinsia, Kadafi alikuwa akimtembelea kila siku. Katika moja ya ziara hizo, Tupac na Kadafi wakaamua kuunda kikundi cha rap cha Outlawz, ambacho kiliundwa kwa lengo la kuwarudisha washiriki wengi kutoka kwa vikundi vya awali vya Tupac, Dramacydal na Thug Life . Fula pia aliungana na mshirika wake wa Outlawz Hussein Fatal kurekodi nyimbo kadhaa chini ya jina "Fatal-N-Felony". Albamu ilipangwa lakini haikutekelezeka, ingawa nyimbo zingine zilizopangwa kwa albamu zilionekana kwenye Son Rize Vol. 1.

Mwaka huohuo, Tupac alipoachiliwa kutoka gerezani, Kadafi alikutana naye kusaini mkataba na studio ya Death Row. Alionekana kwenye nyimbo tatu za albamu ya Tupac, All Eyez. Kipindi hicho, Fula alianza kuingia kuvuta nadhari ya macho ya umma, akionekana kwenye video za muziki, akienda katika sherehe mbalimbali za tuzo za muziki huku akipanda jukwaani kutumbuiza. Akina Outlawz walirekodi mara kwa mara na Tupac kipindi chote cha mwaka wa1996.

Mnamo Septemba 13, 1996, Tupac alikufa baada ya kupigwa risasi mara kadhaa akiwa katika gari-karibu na Ukanda wa Las Vegas mnamo Septemba 7. Kadafi alikuwa ndani ya gari la nyua ya Tupac, na alidai kuwa aliona Cadillac nyeupe ikisimama kando yake na kufyatua risasi. [3]

Kifo[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Novemba 10, 1996, karibu miezi miwili baada ya kifo cha Tupac, Kadafi, akiwa na umri wa miaka 19, alipatikana akiwa amelala katika ngazi ya ghorofa ya tatu ya jengo la ghorofa huko 325 Mechanic Street huko Orange, New Jersey . Kulingana na jarida la Las Vegas Sun, [4] Fula alipatikana na polisi wa New Jersey majira ya saa tisa na dakika 48 za usiku. Inaaminika alipigwa risasi ya kichwa mara moja kwa bahati mbaya na binamu yake Napoleon, Roddy Beale, ambaye baadaye alijisalimisha kwa polisi na kutumikia kifungo cha miaka 7-8. Hata hivyo, hii imekuwa ikibishaniwa sana na mama yake Kadafi na shahidi mwingine wa kike. [5] Kifo chake kimeandikwa katika machapisho mbalimbali ikiwa ni paoja na kitabu cha Cathy Scott kilichoitwa Killing of Tupac Shakur . [6] [7]

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

Albamu za Solo[hariri | hariri chanzo]

  • Son Rize Vol. 1 (2004)

Albamu za ushirikiano[hariri | hariri chanzo]

Kuonekana kama mgeni[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Yaasym Fula interview with Kadafi Legacy". Kadfilegacy. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-03-22. Iliwekwa mnamo March 21, 2014.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. ""IMDb Biography of Yafeu Fula" IMDb". IMDb. Iliwekwa mnamo May 25, 2012.  Check date values in: |accessdate= (help)
  3. "Witness to Rapper's killing is shot dead". Los Angeles Times. November 14, 1996. Iliwekwa mnamo May 22, 2012.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  4. Scott, Cathy (November 13, 1996). "Shakur shooting witness found dead in N.J.". Las Vegas Sun. Iliwekwa mnamo May 22, 2012.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  5. "Napoleon (Outlawz) on his Cousin Accidentally Killing Kadafi". YouTube. DJ Vlad. Iliwekwa mnamo July 14, 2017.  Check date values in: |accessdate= (help)
  6. Scott, Cathy (2002). The Killing of Tupac Shakur. ISBN 9780929712208. Iliwekwa mnamo June 5, 2012.  Check date values in: |accessdate= (help)
  7. "Published books about Yaki Kadafi". Iliwekwa mnamo June 5, 2012.  Check date values in: |accessdate= (help)

 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]