Nate Dogg
Nate Dogg | |
---|---|
Jina la kuzaliwa | Nathaniel Dwayne Hale |
Amezaliwa | Clarksdale, Mississippi, Marekani | Agosti 19, 1969
Amekufa | Machi 15, 2011 (umri 41) Long Beach, California, United States |
Aina ya muziki | Hip hop, West Coast hip hop, R&B, G-funk |
Kazi yake | Rapa, Mwimbaji |
Miaka ya kazi | 1990–2011[1] |
Studio | Death Row Elektra Doggystyle Atlantic |
Ame/Wameshirikiana na | 213, Snoop Dogg, Warren G, 2Pac, Dr. Dre, The Game, Proof, Eminem, 50 Cent, Tha Dogg Pound, Fabolous |
Nathaniel Dwayne Hale (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Nate Dogg; Clarksdale, Mississippi, 19 Agosti 1969 - Long Beach, 15 Machi 2011) alikuwa rapa na mwimbaji wa muziki wa hip hop na R&B kutoka nchini Marekani. Alifahamika sana kwa uanachama wake katika kundi la rap lililokuwa na wasanii watatu la 213 na kazi zake za kujitegemea ambapo amepata kushirikiana na Dr. Dre, Warren G, Tupac na Snoop Dogg katika matoleo kadha wa kadha bab-kubwa ya wasanii hao. Nate Dogg ametoa albamu tatu za kujitegemea, G-Funk Classics, Vol. 1 & 2 mnamo 1998, Music and Me mnamo 2001 na Nate Dogg mnamo 2008.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Nate Dogg alizaliwa mjini Clarksdale, Mississippi. Alihamia mjini Long Beach, California akiwa na umri wa miaka 14 kwa kufuata kuchana kwa wazazi wake. Alikuwa rafiki na mwenza wa katika gumu hili la rap na marapa kama vile Snoop Dogg, Warren G, RBX, Daz Dillinger na binamu yake Butch Cassidy na Lil' ½ Dead. Ameanza kuimba akiwa bwana mdogo katika kanisa la New Hope Baptist Church huko mjini Long Beach na Life Line Baptist Church huko Clarksdale, Mississippi ambapo baba'ke bwana Daniel Lee Hale alikuwa mchungaji katika kanisa hilo. Akiwa na umri wa miaka 16 ameacha shule na kwenda kujiunga na United States Marine Corps,[2] akitumikia kwa miaka mitatu.
Nate Dogg amefariki mwaka wa 2011 huko mjini Long Beach, California; sababu za kufa ni kutokana na utatanishi mbalimbali uliosababishwa na kupooza kwa mwili.[3]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Diskografia
[hariri | hariri chanzo]- G-Funk Classics, Vol. 1 & 2 (1998)
- Music and Me (2001)
- Nate Dogg (2008)
Filmografia
[hariri | hariri chanzo]- The Transporter wimbo "I Got Love" (2002)
- Doggy Fizzle Televizzle akiwa kama mwimbaji wa kibwagizo cha filamu "The Braided Bunch" (2002–2003)
- Head of State akiwa kama jina lake (pia mwimbaji na mtunzi wa kibwagizo cha filamu hii) (2003)
- Need For Speed: Underground wimbo "Keep it Comin"
- The Boondocks (2008)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Bishop Lamont ft Nate Dogg "I'm Faded" [Audio]". 8 Januari 2011. Iliwekwa mnamo 14 Mei 2011.
- ↑ "Joining the Ranks of Famous Marines". USMC.net. Iliwekwa mnamo 26 Desemba 2009.
- ↑ Perpetua, Matthew (16 Machi 2011). "Rapper and Singer Nate Dogg". Rolling Stone. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-05-18. Iliwekwa mnamo 7 Mei 2011.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Nate Dogg at the Internet Movie Database