50 Cent

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
50 Cent
50 Cent, mnamo 2006
50 Cent, mnamo 2006
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Curtis James Jackson III
Amezaliwa 6 Juni 1975 (1975-06-06) (umri 48)
Asili yake Queens, New York

Marekani

Aina ya muziki Hip hop
Kazi yake Rapa
Mwigizaji
Mtayarishaji
Studio Jam Master Jay Records
Columbia Records
Aftermath Records
G-Unit Records
Interscope Records
Shady Records
Violator Records
Ame/Wameshirikiana na G-Unit
Eminem
Dr. Dre
Mobb Deep
Sha Money XL
Tovuti 50cent.com

Curtis James Jackson III (amezaliwa tar. 6 Juni 1975) ni mwanamuziki wa rap-hip hop, mwigizaji na mtayarishaji kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama 50 Cent.

Ameanza kupata umaarufu zaidi baada ya kutoa albamu yake ya "Get Rich or Die Tryin" na 'The Massacre'. 50 Cent amepata Plantinam nyingi na mafanikio makubwa katika albamu zake mbili, aliuza nakala zaidi ya Mil. 21 kwa hesabu ya dunia nzima.

Masha ya awali na muziki[hariri | hariri chanzo]

50 Cent alizaliwa mjini South Jamaica, Queens ndani ya New York, Marekani. 50 Cent ameanza kujishughulisha na masuala ya uuzaji wa dawa za kulevya toka akiwa na umri wa miaka 12, hiyo ilikuwa kwenye miaka ya '80', akiwa anajushughulisha na masuala ya uuzaji wa dawa za kulevya. 50 Cent pia akawa anajaribu kidogo masuala ya muziki wa rap na hip hop.

50 Cent alipigwa risasi tisa mnamo mwaka 2000. Kadri miaka inavyozidi kwenda 50 Cent akabahatika kutoa tepu ya nyimbo mchanganyiko ilyokuwa inaitwa "Guess Who's Back?" mnamo mwaka wa 2002.

50 Cent aligunduliwa kipaji chake na mwanamuziki 'Eminem' na kumwingiza katika studio ya Interscope Records kwa msaada wa Eminem na Dr. Dre, ambaye ndiye aliye tayarisha albamu ya kwanza ya 50 Cent na kumpa mafanikio makubwa katika ulimwengu wa muziki.

Studio binafsi[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka 2003 50 Cent alianzisha Studio yake iitwayo G-Unit Records, ambayo iliingiza Marapa maarufu kama vile Young Buck, Lloyd Banks, na Tony Yayo, kitu ambacho kilipelekea kupata uhasama na chuki nzito na baadhi ya wasanii nchini marekani, moja kati ya wasanii hao ni Ja Rule, The Game, na Fat Joe. Pia 50 Cent alikuwa akiibia masuala ya uigizaji na kuonekana kwenye baadhi ya filamu zenye kuhusu albamu yake na filamu illitwa "Get Rich or Die Tryin" na akashiriki pia kwenye filamu ya "Iraq War" na filamu ya "Home of the Brave" iliyotoka mwaka 2006.

Albamu alizotoa[hariri | hariri chanzo]

Filamu alizotoa[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Jina la Filamu Jina Aliotumia Maelezo
2003 50 Cent: The New Breed 50 Cent Makala za Documentary DVD
2005 "Pranksta Rap" 50 Cent The Simpsons Sehemu ya 16.9
Get Rich or Die Tryin' Marcus Toleo la Motion picture
50 Cent: Bulletproof 50 Cent Video game, Sauti tu.
2006 Home of the Brave Jamal Aiken
2007 The Dance
2008 The Ski Mask Way Seven Ipo kwenye Maandalizi
Righteous Kill Inatengenezwa
Live Bet

Tuzo alizopata[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: