Fabolous
Fabolous | |
---|---|
Fabolous at Sirius Satellite Radio in 2007
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | John David Jackson |
Aina ya muziki | Hip hop |
Kazi yake | Rapa, mtunzi wa nyimbo |
Miaka ya kazi | 1998–mpaka sasa |
Studio | Desert Storm, Def Jam |
Ame/Wameshirikiana na | Jagged Edge, Lil Mo, Nate Dogg, Mike Shorey, Ne-Yo, Pharrell Williams, Red Cafe, The-Dream, Young Jeezy |
John David Jackson (amezaliwa tar. 18 Novemba 1977) ni msanii wa rekodi za hip hop kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina la kisanii kama Fabolous. Alikulia mjini Brooklyn huko New York City, alikuwa mmoja kati marapa wa East Coast ambao waliathiriwa na muziki wa Southern hip hop. Moja kati ya kazi zake za awali ambayo ilimletea umaarufu ni pamoja na "Can't Deny It" mnamo 2001, kutoka katika albamu yake ya kwanza ya Ghetto Fabolous. Fabolous ametoa albamu tano, ambazo zote kwa ujumla zimeuza nakala zaidi ya milioni tatu huko nchini Marekani.[1]
Maisha na kazi
[hariri | hariri chanzo]Maisha ya awali na mwanzo wa kazi
[hariri | hariri chanzo]Fabolous alizaliwa John David Jackson mnamo tar. 18 Novemba 1977, na wazazi wenye asili ya Kiafrika-Kiamerika na Kidominika.[2][3] Alikulia huko Bedford-Stuyvesant jirani kidogo na Brooklyn, New York.[4][5] Wakati anasoma elimu ya juu, Fabolous akaanza kujifua katika masuala ya muziki wa rap. Alialikwa kurap moja kwa moja kipindi cha redio cha DJ Clue na kwenye WQHT Hot 97, ambapo kulimpatia uwezo wa kuweza kuingia mkataba na studio ya Desert Storm Records.[6] Alipata kushirikishwa kwenye mamixi tepu kibao ya DJ Clue na mamixi tepu mengine mingi tu ya wasaniii wa Roc-A-Fella.
Diskografia
[hariri | hariri chanzo]- Ghetto Fabolous (2001)
- Street Dreams (2003)
- Real Talk (2004)
- From Nothin' to Somethin' (2007)
- Loso's Way (2009)
- Loso's Way 2 (2010)[7]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Hilliard, Chloe A. (2008-02-05). "The Fabolous Life". The Village Voice. New Times Media. ku. 1–4. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-01-01. Iliwekwa mnamo 2009-03-01.
- ↑ Birchmeier, Jason. "Fabolous - Biography". Allmusic. Iliwekwa mnamo 2008-10-18.
- ↑ "Fabolous". Hip Hop Galaxy. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-12-08. Iliwekwa mnamo 2008-02-28.
- ↑ Mfuni, Tanangachi; Gould, Joe; Lemire, Jonathan. "Rapper Fabolous' friend is fatally stabbed, according to club area toll", New York Daily News, 2007-11-24. Retrieved on 2008-02-28. Archived from the original on 2009-02-08.
- ↑ Vasquez, Emily. "Brooklyn-Born Rapper Is Arrested After Being Shot", The New York Times, 2005-10-18. Retrieved on 2007-10-07.
- ↑ Reid, Shaheem (2001-05-17). "Fabolous Gets A Clue, Records Debut Album For Mixtape King". MTV News. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-07-25. Iliwekwa mnamo 2009-07-31.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-03-16. Iliwekwa mnamo 2010-02-15.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Official Def Jam Site
- Rich Yung Society Clothing site
- Fabolous Clothing Line Archived 18 Desemba 2014 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Marekani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Fabolous kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |