Ghostface Killah

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ghostface Killah

Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Dennis Coles
Pia anajulikana kama Tony Starks, Ironman, General Tony Starks, Pretty Toney, The Wallabee Kingpin, GFK, Ghost Deini, Starky Love, P Tone, Sun God, Wally Champ
Amezaliwa 9 Mei 1970 (1970-05-09) (umri 53)
Asili yake Staten Island, New York, Marekani
Aina ya muziki Hip hop
Miaka ya kazi 1991–mpaka sasa
Studio Razor Sharp, Epic, Starks Enterprises, Def Jam
Ame/Wameshirikiana na Wu-Tang Clan, Theodore Unit, MF DOOM, Rakim, Adult Swim
Tovuti Ghostface's official site

Dennis Coles (amezaliwa tar. 9 Mei 1970)[1] ni msanii wa muziki wa hip hop kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Ghostface Killah. Huyu ni mmoja kati ya wanaounda kundi zima la Wu-Tang Clan. Baada ya kundi kuambulia mafanikio yake makubwa kwa kutoa albamu yao ya kwanza iliyokwenda kwa jina la Enter the Wu-Tang (36 Chambers) , huyu bwana naye akaamua kujiendeleza mwenyewe akiwa kama msanii wa kujitegemea na kuweza kupata mafanikio kibao. Ghostface Killah akatoa albamu yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la Ironman, ambayo ilipokewa vyema sana na watathmini wa masuala ya muziki. Akaendeleza kazi yake, na kutengeneza albamu zake zilizojishindia tuzo kemekem. Albamu hizo ni pamoja na Supreme Clientele, Fishscale, na The Big Doe Rehab.

Ghostface Killah ni maarufu mno[2][3] kwa staili yake ya sauti kubwa, kuchana kwa haraka-haraka, na staili yake ya kuimba kama hataki huku akiwa anatia mbwembwe za maneno ya kitaa-kistori fulani ya kujitambua.[4][5]

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Ghostface Killah amezaliwa na kukulia mjini Stapleton kwenye nyumba za miradi huko New York. Kwenye wimbo wake wa kujielezea mwenyewe wa "All That I Got Is You", Ghost anaelezea maisha yake ya utoto. Ana rap akielezea jinsi alivyokua kwenye mjengo wa vyumba vitatu vya kulalia bila baba yake, ambaye alimwacha tangu akiwa na umri wa miaka sita.

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

Albamu zake[hariri | hariri chanzo]

Kompilesheni[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Erlewine, Stephen Thomas. Ghostface Killah - Biography. Allmusic. Iliwekwa mnamo 2009-01-03.
  2. Brown, Marisa (2007). The Big Doe Rehab: Review. Allmusic. Iliwekwa mnamo 2009-08-06.
  3. O'Donnell, Mallory (2006-12-14). More Fish. Stylus Magazine. Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-06-21. Iliwekwa mnamo 2009-08-06.
  4. Frere-Jones, Sasha (2006-03-20). Ghost's World. The New Yorker. Iliwekwa mnamo 2009-08-06.
  5. Dombal, Ryan (2006-03-31). Ghost' Writer. EW.com. Jalada kutoka ya awali juu ya 2014-10-12. Iliwekwa mnamo 2009-08-06.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]



Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ghostface Killah kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.