Nenda kwa yaliyomo

Kanye West

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kanye West
Kanye West kunako mwaka 2007.
Kanye West kunako mwaka 2007.
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Kanye Omari West
Amezaliwa 8 Juni 1977 (1977-06-08) (umri 47)
Atlanta, Georgia, Marekani
Asili yake Chicago
Illinois
Marekani
Aina ya muziki Hip hop
Kazi yake Mtayarishaji
Rapa
Mshairit
Mtunzi wa nyimbo
Ala Sauti
Ngoma
Kinanda
Studio GOOD Music
Roc-A-Fella
Def Jam
Ame/Wameshirikiana na Child Rebel Soldier, Jay-Z, Common, Talib Kweli, Consequence, John Legend, Mos Def, Lupe Fiasco, Pharrell, GLC
Tovuti Kanyeuniversecity.com

Kanye Omari West (amezaliwa tar. 8 Juni 1977)[1] ni mshindi mara ishirini na moja wa Tuzo za muziki za Grammy, akiwa kama rapa-mtayarishaji bora wa muziki kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Kanye West.

West alitoa albamu yake ya kwanza mnamo mwaka wa 2004, na albamu ilikwenda kwa jina la The College Dropout. Albamu yake ya pili iliitwa Late Registration na ilitoka mnamo mwaka wa 2005, na pia ikafuatia albamu yake ya tatu iliyotoka mwaka 2007 ikiwa na jina la Graduation.

Albamu zake zote tatu zilipata tuzo kadhaa, umaarufu,[2][3][4] na mafanikio ya kibiashara. West pia anamiliki studio yake mwenyewe iitwayo GOOD Music.[5] Wazazi wa West walitalikiana wakati akiwa na umri wa miaka mitatu, kisha yeye na mama yake wakaamia zao mjini Chicago, Illinois. Alijiandikisha katika Chuo Kikuu cha Chicago lakini baadaye aliacha kujiendeleza na masuala yake ya kazi za muziki.

Alianza kujibebea umaarufu baada ya kutengeneza single kadhaa za muziki. Miongoni mwa single alizofanya ni pamoja na ya Jay-Z, Alicia Keys, na Janet Jackson. Staili nyingi za West katika utayarishaji wake huwa anaweka vielelezo vya sauti vyembamba ambavyo vinaambatana na vigoma na ala tupu za muziki.

Albamu zake

[hariri | hariri chanzo]
Makala kuu ya: Albamu za Kanye West
  1. "Kanye facts!". Channel 4. 2007-08-17. Iliwekwa mnamo 2008-04-26.
  2. "2005 Grammy Award Winners". CBS News. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-06-20. Iliwekwa mnamo 2008-04-24.
  3. "List of Grammy winners". CNN. Iliwekwa mnamo 2008-04-24.
  4. "Kanye West". Metacritic. Iliwekwa mnamo 2008-04-24.
  5. "GOOD Music". GOOD Music. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-04-22. Iliwekwa mnamo 2008-04-24.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kanye West kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.