Jadakiss

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jadakiss

Maelezo ya awali
Amezaliwa 27 Mei 1975 (1975-05-27) (umri 48)
Yonkers, New York, U.S.
Aina ya muziki Hip hop
Kazi yake Rapper
Miaka ya kazi 1993–hadi leo
Studio D-Block, Ruff Ryders, Def Jam
Ame/Wameshirikiana na The LOX, Styles P, Sheek Louch, DMX, Swizz Beatz, Raekwon, Jay-Z, Fat Joe, Rick Ross, Pharrell

Jason Phillips (amezaliwa tar. 27 Mei 1975),[1] anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Jadakiss, ni rapa kutoka nchini Marekani. Huyu ni mwanachama wa kundi zima la The LOX. Jadakiss ni mmoja kati ya wamiliki wa chapa ijulikanayo kama D-Block.

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Akiwa na umri wa 16, Jadakiss alikuwa rapa wa michano huru. Yeye na baadhi ya marafiki zake walipewa fursa ya kushiriki kwenye shindano la "Jack the Rapper Competition" huko mjini Florida, ambapo Jadakiss aligunduliwa kipaji chake cha kupambana kirap. Akakutana na Dee na Wah wa Ruff Ryders (halafu kuongoza kampuni), na kuanza kazi kuzura kimapambano ya michano nje ya studio ya Ruff Ryders ambapo baadhi ya wasanii kama vile DMX wamefanya vibao vyao kwa mara ya kwanza.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Jadakiss ameanzisha kundi la The Warlocks kunako mwaka wa 1994 akiwa na washkaji zake Sheek Louch, Chris "Lil Mac" Pelkey, na Styles P. Baadaye wakaingia mkataba na Bad Boy Entertainment, ambapo walishauriwa kubadili jina lao liwe fupi kuwa "The LOX", ambayo inasimama kama Living Off eXperience. Wameanza kuonekana kwa mara ya kwanza mnamo mwaka wa kwenye LP ya The Main Source mnamo 1994 Fuck What You Think katika wimbo wa "Set it Off".

Kundi, hasa Jadakiss, amejenga uhusiano wa karibu sana na The Notorious B.I.G., kipindi hicho Jadakiss yupo begani mwa Biggie. Kibao cha kwanza cha The LOX kilitolewa kama ukumbusho wa Biggie kiliitwa "We'll Always Love Big Poppa" (upande wa pili wa wimbo wa Puff Daddy "I'll Be Missing You") mnamo 1997.Mwaka wa 1998, kina LOX wametoa kibao cha Money, Power & Respect. Baada ya albamu hii, wameondoka Bad Boy Records.

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

Studio albums

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Smith, Kerry L. (2004). Jadakiss > Biography. allmusic. Iliwekwa mnamo 20 Oktoba 2008.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]