Nenda kwa yaliyomo

Runnin' (Dying to Live)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kwa wimbo wa 2Pac na The Notorious B.I.G. wa mwaka wa 1994, tazama Runnin'
“Runnin' (Dying to Live)”
“Runnin' (Dying to Live)” cover
Single ya 2Pac akimshirikisha The Notorious B.I.G.
kutoka katika albamu ya Tupac: Resurrection Soundtrack
Imetolewa 2003
Muundo CD
Imerekodiwa Miaka ya 1990-2003
Aina Hardcore Hip hop, Gangsta Rap
Urefu 3:51
Studio Amaru
Mtunzi Tupac Shakur
Christopher Wallace
Mtayarishaji Eminem
Mwenendo wa single za 2Pac akimshirikisha The Notorious B.I.G.
"Still Ballin'"
(2002)
"Runnin' (Dying to Live)"
(2004)
"One Day at a Time (Em's Version)"
(2004)
Mwenendo wa single za The Notorious B.I.G.
"Dead Wrong"
(1999)
"Runnin' (Dying to Live)"
(2004)
"Nasty Girl"
(2005)

"Runnin' (Dying to Live)" ni wimbo ulioimbwa na 2Pac na The Notorious B.I.G.. Wimbo ulitoka wa kwanza kutolewa kama single kutoka katika albamu ya Tupac: Resurrection. Video yake imejumlisha mahojiano ya wote wawili, yaani, Tupac na Biggie. Pia, ni wimbo pekee kutoka katika albamu kuwa na muziki wa video. Kiitikio cha wimbo kinatoka katika wimbo wa Edgar Winter wa "Dying to Live" (kutoka katika albamu ya Edgar Winter's White Trash), ambayo ilirekodiwa kwa kasi ya juu kwa ajili wimbo huu. Wimbo ulishika nafasi ya #19 kwenye chati za Billboard Hot 100. Tupac Shakur na Biggie Smalls awali waliurekodi wimbo huu wakiwa pamoja mnamo 1994. Awali wimbo ulitayarishwa na mtayarishaji wa New York Easy Mo Bee na uliitwa "Runnin' (From tha Police)". Mahojiano ya Biggie yalirekodiwa siku mbili tu kabla ya kifo chake.

Toleo la video linazima sauti ya lugha zote, fujo na marejeleo ya dawa za kulevya, hata maneno ya Biggie kuhusu 2Pac kupigwa risasi tena (toleo la redio limeweka yote kasoro neno "bitches" kwenye mstari wa 2Pac). Video, ina sehemu kadhaa ya taswira za 2Pac na Biggie, na pindi mistari yao inapoisha, sauti inaonekana kupungua chini zaidi. Sehemu ya wimbo ya 2pac haipo sawa na sehemu ile ya kwenye Runnin' (From tha Police).


UK CD single
# JinaMtunzi (wa)Watayarishaji Urefu
1. "Runnin' (Dying to Live)" (feat. The Notorious B.I.G.) Eminem 3:51
2. "Still Ballin'" (Nitty remix) Nitty 2:49