Nenda kwa yaliyomo

Brenda's Got a Baby

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“Brenda's Got a Baby”
“Brenda's Got a Baby” cover
Single ya 2Pac akishirikiana na Dave Hollister
kutoka katika albamu ya 2Pacalypse Now
Imetolewa 9 Oktoba 1991
Muundo 12" single
Imerekodiwa 1991
Aina Hip hop ya kisiasa
Urefu 3:55
Studio Interscope
Mtunzi T. Shakur, D. Evans
Mtayarishaji The Underground Railroad
2Pac singles 2Pac akishirikiana na Dave Hollister
"Brenda's Got a Baby"
(1991)
"If My Homie Calls"
(1991)

"Brenda's Got a Baby" ni jina la kutaja single ya kwanza ya rapa Tupac Shakur, na ni wimbo wa kumi kutoka katika albamu yake ya kwanza ya 2Pacalypse Now. Wimbo huu, ambao umemshirikisha mwimbaji wa R&B Dave Hollister, ina-mhusu msichana mmoja aliyeitwa Brenda ambaye anaishi ghetto, ana mtoto, na hana uwezo wa kujikimu ili amsaidie mtoto wake. Wimbo unaelezea hasa masuala ya upataji mimba kwa vijana wadogo na athari za kuwa mama ukiwa mdogo na familia zao. Kama jinsi ilivyo katika nyimbo nyingi za Shakur, "Brenda's Got a Baby" inaelezea maisha ya watu waliokuwa maskini wa kutupwa. Anatumia jina la Brenda kuwakilisha akina mama wadogo wote kwa ujumla, Shakur ameponda sana kiasi kidogo cha msaada kutoka kwa baba wa mtoto, serikali, na jamii kwa ujumla. Shakur ametunga wimbo huu baada ya kusoma makala ya gazeti moja inayomhusu msichana mmoja mdogo mwenye umri wa miaka kumi na mbili kwamba amepata uja-uzito kutoka kwa binamu yake, na kwa sababu hakutaka wazazi wake wajue kama ana-mtoto, ameamua kumtupa jalalani.