The Fix (Heroes)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
"The Fix"
Sehemu ya Heroes
Sylar na Mr. Bennet wanakutana uso-kwa-uso
Sylar anamzingua Mr. Bennet baada ya kujitia kafa.
Sehemu ya. Msimu 1
Sehemu 13
Imetungwa na Natalie Chaidez
Imeongozwa na Terrence O'Hara
Tayarisho la 113
Tarehe halisi ya kurushwa 29 Januari 2007
Waigizaji wageni
Wendo wa sehemu
← Iliyopita Ijayo →
"Godsend" "Distractions"
Orodha ya sehemu za Heroes

"The Fix" ni sehemu ya kumi na tatu ya msimu wa kwanza wa mfululizo wa igizo la ubunifu wa kisayansi linalorushwa hewani na kituo cha televisheni cha NBC, Heroes.

Hadithi[hariri | hariri chanzo]

Niki bado yupo kwenye jela ya wilaya. Bingwa wa maono anawasili ili aweze fanyakazi juu ya kesi ya Niki, na kumtibu mardhi yake ya uwili-uwili, lakini Niki kakataa msaada wake. Muda huohuo, D.L. ana hali ngumu katika upataji wa fedha ilimradi aweze kulipa kodi ya pango, na kuwa baba peke yake kwa Micah.

Kanyata hadi kwenye selo ya Niki ili amtoroshe, lakini aliendelea kusisitiza abakie pale na kumwambia ajikaze hivyohivyo na aendelee kumtunza Micah. Baada ya kutoka shule, Micah kasimama kwenye kituo cha ATM na kutumia nguvu zake kutoa maelfu ya madola. D.L. na Micah wanaelewana, na Micah anampatia baba'ke fedha akalipe kodi ya pango. Mwanasaikolojia anarudi kumsaidia Niki, lakini ili amsaidie Niki, Niki lazima amwache azungumze na Jessica.

Matt anamweleza mkewe kuhusu matukio yalitokea kwenye kiwanda cha makaratasi cha Primatech. Yu katika hali ngumu sana kukubali nguvu zake na matukio ya miezi kadhaa iliyopita. Pia anamwomba atengeneze bomba.

Amehudhuria kwenye tahakiki yake, ambapo maelezo yake ya tukio halisi la Primatech hayajaaminiwa na viongozi watatu. Matt kafirikia upya na kusema kwamba kaongopa kwa sababu alifeli mara tatu kwenye majaribio yake ya uaskari mpelelezi na hivyo anataka aonekane kama shujaa. Bodi ya utahakiki imemsimamisha kazi kwa muda wa miezi sita. Amerudi nyumbani na kukuta bomba linavuja.

Baada ya kutengeneza bomba, anamwambia mkewe kuhusu kusimamishwa kazi kwake, akihofia kwamba tayari keshavurugwa na ndoa imeharibika. Mkewe kamwacha asome akili yake kwa mara nyingingine tena. Matt kafanya hivyo na kugundua kama mkewe ni mjamzimto. Furaha imerudi tena.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]