The Hard Part

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
"The Hard Part"
Sehemu ya Heroes
Heroes s01e21.jpg
Hiro anapambana na Sylar.
Sehemu ya. Msimu 1
Sehemu 21
Imetungwa na Aron Eli Coleite
Imeongozwa na John Badham
Tayarisho la 121
Tarehe halisi ya kurushwa 7 Mei 2007
Waigizaji wageni
Wendo wa sehemu
← Iliyopita Ijayo →
"Five Years Gone" "Landslide"
Orodha ya sehemu za Heroes

"The Hard Part" ni sehemu ya ishirini na moja ya msimu wa kwanza wa mfululizo wa kipindi cha ubunifu wa kisayansi kinachorushwa hewani na televisheni ya NBC, Heroes. Ni sehemu ya kwanza katika sehemu tatu za mwisho za msimu wa kwanza.[1] Jina linatokana na mstari wa mwisho wa Hiro kwenye sehemu iliyopita, "Now the hard part." Pia ni mstari wa kwanza kwenye kipengele hiki.

Hadithi[hariri | hariri chanzo]

Kwenye mkesha wa uchaguzi, matukio yanaendelea kutoa wahusika huko mjini New York City. Kwenye karakana ya Isaac Mendez, Sylar anaendela kuchora. Akiangalia matokeo, anaona mchoro wa mapambano baina yake yeye na Ted Sprague, na mlipuko mwingine wa nyuklia huko mjini New York. Anagundua ya kwamba huenda akawa ndiye chanzo cha mlipuko, Sylar anampigia simu Mohinder Suresh na kuomba msaada wake, anasema kwamba hataki kuua watu wasio na hatia, na kwamba amechukua nguvu kutoka kwa watu ambao "hawa-kustahili kuwa nazo" - lakini kisha akakata simu baada ya kumsikia Mohinder anapiga '911' kupitia simu yake ya mkononi. Sylar kisha anampigia mama'ke, Virginia Gray (Ellen Greene), na kumwuliza kama anaweza kwenda kumuona.

Mohinder anakutana na Thompson, ambaye pia kwa mara ya pili anajaribu kumshawishi ajiunge na kikosi. Mohinder amesita, na kusema kwamba wao wote ni wahuni. Thompson bado anang'ang'ania, anamtambulisha Mohinder kwa Molly Walker, msichana mdogo mwenye uwezo wa kutazama mbali na kuona kila mtu alipo hataka kama yupo wapi. Hata hivyo, hawezi kutumia uwezo huu kwa kufuatia uchache wa ugonjwa uliomuua dada'ke Mohinder, Shanti.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Lee, Patrick (2007-03-19). Heroes Finale Details Leaked. SciFi Wire. Iliwekwa mnamo 2007-03-19.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]