Hiros

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
"Hiros"
Sehemu ya Heroes

D.L. amerudi.
Sehemu ya. Msimu 1
Sehemu 5
Imetungwa na Michael Green
Imeongozwa na Paul Shapiro
Tayarisho la 105
Tarehe halisi ya kurushwa 23 Oktoba 2006
Waigizaji wageni
Wendo wa sehemu
← Iliyopita Ijayo →
"Collision" "Better Halves"
Orodha ya sehemu za Heroes

"Hiros" ni sehemu ya tano ya msimu wa kwanza wa mfululizo wa igizo la ubunifu wa kisayansi linalorushwa hewani na kituo cha televisheni cha NBC, Heroes.

Hadithi (kwa ufupi)[hariri | hariri chanzo]

Claire[hariri | hariri chanzo]

Claire na Brody wameponyeka kwenye ajali yao na wanaonekana hospitalini. Claire mwishowe kaamua kumweleza baba yake kwamba Brody alijaribu kumbaka, lakini akamtaka amwahidi hatouambia uongozi. Japokuwa Mr. Bennet ameahidi hatomwambia mtu yeyote, baadaye anaonekana kutembelea chumba cha Brod wakiwa na mtu asiyejulikana. Brody anatishia kumshtaki baba wa Claire, lakini Mr. Bennet anamweleza Brody aliyedhoofika kwamba atampa nafasi zaidi ya kujirekebisha na tabia zake za kishenzi. Ingawa Brody amekataa, yule mtu asiyejulikana ameweza kufuta kumbukumbu zote za Brody. Baadaye, Claire kamtembelea Brody, na kugundua kwamba hamjui hata yeye ni nani, tena hajui hata jina lake.

Matt[hariri | hariri chanzo]

Janice Parkman ana hofu juu ya mumewe aliyepotea, lakini hofu imegueka kuwa jazba pindi alipomgundua anamka kwenye kochi lao. Wakati Matt anaamka kwenye kochi lake, anakumbuka kama alikuwa akifanyakazi na FBI, lakini hakumbuki wapi alipokuwa kwa takriban siku mbili zilizopita. Akisoma fikra za mkewe, Matt alishangzwa kugundua kwamba ni kiasi gani Janice bado ana hofu na kumjali, japokuwa hawana mazungumzo mazuri kabisa. Matt, anasoma fikra za mke wake, ameweza kujua matanio yake na mawazo juu ya ndoto za kweli za mahusiano yao. Akaanza kutenda kwa mujibu wa matakwa yake - basi japo hata moja katika hayo, kama vile kwenda kumnunulia kahawa na ice cream anazozipenda. Matt akatoka kuchukua ice cream. Pindi alipofika dukani, Matt akagundua kuna mwizi anapanga kupora vitu kwa kutumia silaha. Matt ameweza kumshawishi mwizi yule aache suala lile, lakini wateja kwenye duka lile wakamfikiria yeye kama mwizi na akazongwa na mafikra rundo yanatoka kwa wateja wale Matt. Ameishia kwa kuondoka zake tu pale.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]