Company Man
"Company Man" | |||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|
Sehemu ya Heroes | |||||||
Wakina Bennet wanaungana tena baada ya mlipuko. | |||||||
Sehemu ya. | Msimu 1 Sehemu 17 | ||||||
Imetungwa na | Bryan Fuller | ||||||
Imeongozwa na | Allan Arkush | ||||||
Tayarisho la | 117 | ||||||
Tarehe halisi ya kurushwa | 25 Februari 2007 | ||||||
Waigizaji wageni | |||||||
|
"Company Man" ni sehemu ya kumi na saba ya msimu wa kwanza wa mfululizo wa kipindi cha ubunifu wa kisayansi kinachorushwa hewani na televisheni ya NBC, Heroes. Ni kipenge cha kwanza cha Heroes kutelekeza muundo kamili wa hadithi na kufululiza kwenye hadithi moja tu, muundo ambao haujarudiwa tena hadi kwenye msimu wa 3 "Vita Baridi". Kwa maana hiyo, washiriki wengi wa kawaida hawajonekana kwenye kipengele hiki.
Hadithi
[hariri | hariri chanzo]Kipengele hiki kinaelezea pande mbili kuhusu teka nyumbani kwa Bennet na vikumbusho vya Noah Bennet wakati anafanyakazi Primatech.
Vikumbusho
[hariri | hariri chanzo]Kikumbusho cha kwanza kinaonesha Bennet kama anaanza kazi yake ya kificha undani wa Primatech Paper Company. Bosi asiyejulikana wa Bennet, Thompson, anamtaarifu kwamba kila wakala ana mwenzake ambaye ana nguvu za ajabu. Mwenzi wa Bennet ni Claude, ambaye nguvu zake ni za kutoonekana kwa hiari.
Katika kikumbusho kingine, kunaoneshwa mtoto anayekabidhiwa kwa Bennet juu kabisa ya jengo la Deveaux mjini New York. Bennet, Claude, na Kaito Nakamura wanazungumza kwa Kijapani, na Mr. Nakamura anasema kuwa mtoto, "Ni mali yetu. Iwapo akibainika, tunamchukua." Pia kunaoneshwa Hiro Nakamura wakati yungali mdogo sana amekaa pembeni, akicheza mchezo wa video.
Kikukumbusho kingine kinachukua nafasi nje ya nyumbani kwa Bennet, ambapo Bennet anamweleza Thompson kwamba mkewe ameanza kuwa na mashaka kuhusu kazi yake. Thompson anamweleza Bennet kwamba kuna mtoto kagundulika huko nchini Haiti ambaye yeye ana uwezo wa kufuta kumbukumbu. Kwa mara ya kwanza katika mara zote, Bennet ana mruhusu the Haitian aingie nyumbani kwake aende kufuta mashaka ya mkewe.
Katika kikumbusho kingine, Bennet yupo chini ya agizo la kumwua Claude kwa kuvunja usalama wa kumficha mtu mwingine mwenye uwezo. Claude hakushangazwa, kwa vile alikuwepo kwenye ofisi ya Bennet, aonekani, wakati agizo linatolewa. Wakiwa wawili wakasimamisha gari juu ya daraja, Claude anatoa pointi zilezile kwamba Bennet anafanya kitu kilekile cha kumlinda Claire. Lakini wapi Bennet anamtandika risasi Claude, ambaye alipotea na Bennet amehakiki kwamba mwili wake ulianguka chini ya daraja.
Kwenye kikumbusho cha mwisho, Bennet anajaribu kuvaa miwani, anamwuliza binti yake Claire ushauri wake. Claire anashangaa iwapo siku atahitaji miwapi pia, ikiwa wote babu na baba walihitaji miwani. Bennet anatoa siri ya kwamba yule si mwanawe wa kumzaa - bali mlezi tu, kitendo ambacho kilimsikitisha kwa mara ya kwanza. Alimwakikishia kwamba wao ni familia yake ya ukweli. "Hujakulia kwenye tumbo la uzazi wa mama'ko, umekulia kwenye mioyo yetu." Claire anampa miwani aliyoona inamfaa baba'ke ajaribu kuvaa. Pale Bennet alipomwuliza Claire anaonekanaje, anajibu, "Kama baba'ngu."
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Watch "Company Man" at NBC.com
- Beaming Beeman: Episode 17: Company Man - Director's blog on the filming of this episode.