Seven Minutes to Midnight (Heroes)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
"Seven Minutes to Midnight"
Sehemu ya Heroes

Mohinder ana ndoto za ajabu - zinazofanana na ukweli kuhusu Sanjog Iyer.
Sehemu ya. Msimu 1
Sehemu 8
Imetungwa na Tim Kring
Imeongozwa na Paul Edwards
Tayarisho la 108
Tarehe halisi ya kurushwa 13 Novemba 2006
Waigizaji wageni
Wendo wa sehemu
← Iliyopita Ijayo →
"Nothing to Hide" "Homecoming"
Orodha ya sehemu za Heroes

"Seven Minutes to Midnight" ni sehemu ya nane ya msimu wa kwanza wa mfululizo wa igizo la ubunifu wa kisayansi linalorushwa hewani na kituo cha televisheni cha NBC, Heroes.

Hadithi[hariri | hariri chanzo]

Mohinder anarudi India kutawanya majivu ya baba yake. Anajijadili, je, arejee kazi yake kama profesa wa chuo. Msichana wake wa zamani Mira anamwalika kwenye majaribio ya kazi katikia kampuni ya utafiti wa vinasabai ambapo yeye atachaguliwa kuwa mkuu wa kitengo. Hata hivyo, anasema ni lazima asitaje tafiti za baba'ke kuhusu mageko ya nguvu za ajabu au hata kuthubutu kuendeleza sera za utafiti wa namna hiyo kwenye kitengo.

Anaelekea kwenye ofisi ya baba'ke, Mohinder anaona programu inatembea kwenye kompyuta; baada ya bonyeza futa, ujumbe unamwuuliza "are you sure you want to quit" unatokea kwenye kioo na Mohinder anasita kuchagua "yes". Mohinder anazungumza na mama'ke kuhusu uamuzi wake wa kumruhusu baba'ke aende Marekani kumtafuta Sylar. Kwa mara ya kwanza mama yake ana mwambia kuhusu dada yake , Shanti, ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka mitano, miaka miwili baada ya Mohinder kuzaliwa.

Shanti alikuwa wa "namna ya pekee", kwa mujibu wa mama'ke, na baba yao alimpenda sana Shanti kiasi kwamba alihofia Mohinder angegundua mapenzi yake na angetaka usawa. Pia Mohinder anamfululizo wa ndoto, zinamwonesha bwana mdogo wa Kihindi ambaye anamwongoza kwenye matukio kadha wa kadha ikiwa ni pamoja na kumwonesha hata mauaji ya baba'ke kwenye taxi na mtu ambaye sura yake imefumbwa, lakini amevaa saa iliyovunjika kioo, ikionesha saa sita na dakika saba usiku.

Ndoto nyingine ni pale bwana mdogo alipokuwa akijaribu kuingia kwenye sanduku la kwenye meza ya Mohinder, Mohinder kaona funguo kwenye kabrasha la baba'ke ambayo ilikuwa ndani ya lile droo, na kulifungua, na kukuta faili lililoitwa "SANJOG, Iyer", likiwa na picha ya bwana mdogo yule.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]