D. L. Hawkins

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
D. L. Hawkins
muhusika wa Heroes
Mwonekano wa kwanza "Hiros"
Mwonekano wa mwisho "Four Months Ago..."
Imechezwa na Leonard Roberts
Maelezo
Kazi yake Zima moto
Ndoa Niki Sanders
Watoto Micah Sanders
UwezoPhasing

Daniel Lawrence "D. L." Hawkins ni jina la kutaja uhusika uliochezwa na Leonard Roberts kwenye mufululizo wa kipindi cha TV cha Heroes. Huyu ni baba wa Micah Sanders na mume wa Niki Sanders, ana uwezo wa kupitia katika vitu vigumu, yaani, ukuta na kadhalika, tena bila hata kupata madhara yoyote yale.

Historia yake[hariri | hariri chanzo]

Katika miezi sita ya awali na matukio zaidi ya mfululizo, D. L. alikuwa mfanyakazi wa ujenzi. Yeye na mkewe Niki walikuwa na shida ya fedha na kazi ya ujenzi haikuwa inamlipa vyema. Wakati fulani, wametafakari kumwachia familia baba wa Niki, Hal Sanders, katika maisha yao. Kwa sababu yeye amepata mafanikio makubwa sana katika soko la hisa, Hal ameonekana kama anaweza kuwa babu mzuri na ana uwezo wa kutoa msaada wa kifedha. Hata hivyo, punde wanatambua kwamba yungali mnyanyasaji kama awali, ana jazba za haraka kiasi kwamba Niki amethubutu hata kumsahau na kuto-mkubali arudi tena katika maisha yao.

Wakati fulani, D. L. ameanza kuongoza kundi la wahalifu ambao wanavaa mapete yenye fuvu. Hatimaye, ameondoka kundini kabla hawajaiba dola milioni mbili na kumuua mlinzi wa usalama, lakini alitiwa mbaroni kwa uhalifu huo. Amekerwa na mapolisi na hali halisi aliyonayo, anajigundua kama ana uwezo wa kupita katika mahali pagumu bila madhara yoyote. Japokuwa hakuhesabia kama ndiyo uhuru wake, D. L. ametumia nguvu yake kutorokea jela kwa matumaini ya kwamba atasafisha jina lake na kuitunza familia yake.

Katika sehemu ya tatu, mama yake (Paulette Hawkins) na mtoto wake walikuwa wakiwasiliana dhahiri. Pia waliamini kwamba yeye hahusiki na tukio lile la kijambazi, ingawa Niki alikuwa hana uhakika. Mama wa D.L. Bi. Paulette alikamatwa na The Company wakati fulani baada ya hili kutokea.