Angela Petrelli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Angela Petrelli
muhusika wa Heroes
Mwonekano wa kwanza "Genesis"
Mwonekano wa mwisho "The Art of Deception"
Imechezwa na Cristine Rose Alexa Nikolas (Kijana)
Maelezo
Kazi yake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Company
Ndoa Arthur Petrelli
KipawaUotaji uliokua, kupelekea:
  • Ndoto za kiutabiri
  • Udanganyifu wa kindoto

Angela Petrelli (jina kabla ya ndoa ni Shaw), imechezwa na Cristine Rose, ni jina la kutaja uhusika wa tamthilia ya Heroes kupitia televisheni ya NBC. Huyu ni mama wa Nathan na Peter Petrelli. Uhusika huu unatokana na uhusika wa Angela Lansbury - Mrs. Iselin katika filamu ya The Manchurian Candidate.

Katika hali zote mbili, uhusika mkuu huu mwenye ajenda ya siri na matamanio makubwa ya kumfanya awe rais kwa gharama yoyote ile.[1] Ana kipawa cha kuona mustakabali na yale yote yaliyopita kwa kutumia ndoto tu, na pia ana uwezo wa kuingia na kurubuni ndoto za watu wengine. Hili halikujulikana hadi kipindi hiki kilipofika katika msimu wa tatu. Angela alicheza kama adui mkubwa katika mfululizo huu.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Commentary for "How to Stop an Exploding Man"