Nenda kwa yaliyomo

Claire Bennet

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Claire Bennet
muhusika wa Heroes

Hayden Panettiere kama Claire Bennet.
Mwonekano wa mwisho "Brave New World"
Imechezwa na Hayden Panettiere
Maelezo
Majina mengine Claire Butler
UwezoKujiponya majeraha kwa haraka zaidi

Claire Bennet ni mhusika mkuu kwenye igizo la mfululizo wa bunilizi ya kisayansi ya TV ya NBC, Heroes. Uhusika umechezwa na Hayden Panettiere na ameanza kuonekana kwenye televisheni kwa mara ya kwanza katika sehemu kuu ya kwanza kabisa ya mfululizo, "Genesis" mnamo 25 Septemba 2006. Huyu ni mkuu wa mashabiki wa shule-ambaye-amegeuka na kuwa kachero mwenye nguvu ya kujiponesha seli zake kwa haraka zaidi.

Historia yake[hariri | hariri chanzo]

Claire alizaliwa na Nathan Petrelli na Meredith Gordon, watu wawili wenye vipawa. Noah Bennet na mwenzake, Claude, ambao ni makachero wa Kina Company, wanawasili nyumbani kwa Meredith na kumteka-nyara. Claude anaingia ndani na kutengeneza mazingira ya uhalifu ionekane kama ajali wakati Noah yupo nje anasubiri mpaka Meredith apambe moto na kulipua mlango ufunguke. Noah anakimbilia ndani na kumkuta Claude akiwa chini ya sakafu. Claude kisha anamweleza Noah amtafute Claire.

Noah amempata Claire na kumtoa nje akiwa salama. Noah na mkewe, Sandra, baadaye wakamlea Claire. Kwenye riwaya ya picha, "Mkataba wa Kwanza wa Elle, ambao unachukua nafasi kabla ya mfululizo kuanza, Bob anampa Elle kazi mkataba wa kwanza, ambao ni kumfuatilia Claire, huku akijifanya kama mwanafunzi katika shule ya Union Wells High School. Elle akasita, lakini Bob anamhabarisha kwamba Claire ni muhimu sana kwa kina Company na hivyo damu yake yaweza kuwa muhimu sana. Claire hakutambua kwamba Elle anamfuatilia.

Miezi sita ya awali - mwanzoni kabisa mwa mfululizo, Claire amekuwa mkuu wa mashabiki huko shuleni kwake, kwa msaada wa rafiki yake aitwaye Jackie Wilcox. Wakati wa mgogoro wa kugombania mchezo na Jackie, Claire kajigonga kwenye mkoba wa kioo na kujikata mkono. Wakati wanawaoneshea wazazi wa Claire, Bi. Bennet anasema kwamba Claire huenda akahitaji kupigwa nyuzi. Baada ya Claire, Jackie, Bi. Bennet wanaenda hospitalini, simu ikaita na Mr. Bennet akaipokea. Kumbe ni Chandra Suresh, mwanasayansi ambaye ana-somea mambo ambayo si ya kawaida , anamtaarifu kuhusu nguvu za Claire.

Siku kadhaa baadaye, Mr. Bennet anamuuliza kama anaweza kuona zile nyuzi za mkononi mwa Claire. Pale walipotoa kitambaa alichozungushia mkononi mwake - wote wakashangazwa kuona kwamba hakuna hata alama ya mchubuko mdogo mkono mwake.

Baada ya kutambua ile hali ya uwezo usio wa kawaida Claire anaamua kufanya vitu vya hatari huku akiwa na kijana mmoja ambaye ana rekodi matukio yote anayoyafanya.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]