Matt Parkman
Matt Parkman | |
---|---|
muhusika wa Heroes | |
Mwonekano wa kwanza | "Don't Look Back" |
Mwonekano wa mwisho | "Brave New World" |
Imechezwa na | Greg Grunberg |
Maelezo | |
Kazi yake | Afisa wa Polisi Mlinzi Polisi mpelelezi |
Ndoa | Janice Parkman |
Watoto | Matt Parkman Jr. |
Uwezo | Kusoma mawazo ya wengine, kutokea:
|
Matthew "Matt" Parkman, Sr., ni jina la kutaja uhusika wa tamthilia ya katika kipindi cha ubunifu wa kisayansi kinachorushwa hewani na TV ya NBC, Heroes. Uhusika umechezwa na Greg Grunberg. Matt ni afisa wa polisi, ambaye anafanya kazi katika LAPD na NYPD kwenye msimu wa Kwanza na wa Pili. Uwezo wake una mruhusu kusoma mawazo ya wengine, na hatimaye inakua kufikia kiasi cha kuweza hata kudhibiti mawazo ya mtu mwingine, kama ilivyoelezwa na Bob Bishop.
Hadithi
[hariri | hariri chanzo]Genesis
[hariri | hariri chanzo]Matt Parkman ni afisa wa polisi anayefanya kazi na LAPD. Alijaribu kuwa polisi mpelelezi, lakini amevurunda mara tatu kwa kutokana na kwamba hajui kusoma vizuri. Parkman ni msoma-mawazo; anaweza kusikia fikra za watu aliozungukwa nao. Kugundua kwake kwa mara ya kwanza ni baada ya kusikia mawazo ya Molly Walker, msichana aliyejificha asiuawe na mwuaji mkatili aliyeitwa Sylar.
Baada ya kuthibitisha uwezo wake kwa mshirika wake ambaye ni FBI kwa kusoma fikra zake, amepewa nafasi katika upelelezi wa mauaji ya wazazi wake Molly. Mambo yanageuka kuwa hatari baada ya mtu mmoja kutokea kuwa ni Sylar. Wakithubutu kuzuia hatari ya kujeruhiwa kwa Molly, Matt anajaribu kumpoza Molly, wakati Audrey, kachero wa FBI, anamkimbiza Sylar. Hatimaye, yule kafanikiwa kutoroka, lakini kabla hajajionesha sura yake kwa kikamilifu. Baadaye, Matt anarudi nyumbani kwa mke wake, Janice Parkman.